Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Elimu ya Masafa kuwajengea uwezo Madiwani

Imewekwa tar.: September 25th, 2018

Madiwani kote nchini wataanza kupata mafunzo ya uongozi kwa njia ya masafa kupitia mtandao wa kielektroniki, yaani kupitia mfumo wa intaneti, hali itakayowawezesha kujiimarisha katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku na kuwatumikia wananchi.

Akitoa mada jana katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini unaofanyika katika jiji la Dodoma, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria, Dkt. Adephonce Fuka, alisema shabaha ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo yao.

 Dkt. Fuka alisema lengo ni kuhakikisha Madiwani wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni zinazoongoza mabaraza ya madiwani, na mafunzo hayo ni maboresho ya kitabu cha rejea ya Mh. Diwani kilichotumika kufundisha Madiwani kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa 93 hapo awali.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa mtindo wa Elimu-Masafa ili kuwezesha kujifunza mahali popote, yataendeshwa na Chuo cha Serikali za Mitaa - Hombolo, na  ni marejeo ya mafunzo ya awali ambayo yalitolewa kwa viongozi hao kwa Halmashauri 93 zilizopo chini ya mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kutolewa kwa wasilisho la elimu hiyo ya masafa kwa njia ya kieletroniki, mwakilishi kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima, alisema mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), unafanya kazi katika mikoa 13 na Halmashauri 93 na tayari umejipanga kutoa elimu kwa madiwani nchi nzima.

“Mradi huu ni wa miaka mitano, na moja ya maeneo tunayoimarisha ni mfumo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia.  Katika hili, Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo ndio wanaoongoza kipengele cha kutoa mafunzo kwa madiwani, kwani madiwani ndio wawakilishi wa wananchi walio ngazi ya chini kabisa,” alisema Dkt. Kilima.

Dkt. Kilima alisema kuanzishwa kwa utaratibu wa kufundisha kwa masafa (Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki – MUKI) unalenga kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi, gharama nafuu na kwa ufanisi zaidi, tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati wanaanza.

Mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa madiwani yatajikita zaidi katika mada za historia na uhalali wa kisheria wa Serikali za Mitaa, sheria za uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Muundo, Majukumu na Madaraka ya Serikali za Mitaa, sambamba na uendeshaji vikao vya kamati na mikutano ya Baraza.

Muongozo huo utakaokuwa unatoa elimu kwa masafa na kupatikana vilevile kupitia simu ya mkononi, utaangazia suala la utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi, maadili ya madiwani, uibuaji, upangaji na usimamizi wa miradi shirikishi kwenye jamii, sambamba na usimamizi wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Maeneo mengine ni, usimamizi wa raslimali watu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, usimamizi na udhibiti wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, wajibu, majukumu, haki na stahiki za Diwani, pamoja na masuala mtambuka katika jamii.


Anaandika Atley Kuni- OR TAMISEMI.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.