Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

DMDP II KUJENGA BARABARA, MASOKO NA STENDI DAR ES SALAAM

Imewekwa tar.: February 20th, 2024

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) awamu ya pili utajenga barabara za lami katika Mkoa wa Dar es salaam kilomita 250, kuanzisha mfumo wa udhibiti wa taka ngumu, masoko 18 pamoja na vituo vya mabasi tisa.

Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo leo Februari 20, 2024 jijini Dar es salaam kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa fedha za mradi huo  kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia ambapo waliotia saini ni Waziri wa Fedha na Mpango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete.

Akizungumza baada ya kusainiwa mikataba hiyo, Waziri Mchengerwa amesema Jiji hilo limekuwa na changamoto ya miundombinu, ikiwamo ya barabara, ambapo awamu ya kwanza ya DMDP iliboresha jumla ya kilometa 207 katika Halmashauri tatu zilizokuwa chini ya mradi na imeleta  mabadiliko makubwa.

"Sasa hivi mradi huu utatekelezwa  kwenye halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kila halmashauri itajengewa barabara za lami,  masoko pamoja na vituo vya mabasi, mradi unaenda kuangalia changamoto ya usimamizi wa taka ngumu katika Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla wake."

"Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya taka kutochukuliwa kwa wakati na vilevile makandarasi wa kukusanya taka ngumu kuwa na mazingira ambayo sio rafiki kwa kufanya majukumu yao kwa ufanisi, mradi huu unatarajiwa kuboresha miundombinu ya taka ngumu kwa maana ya kuanzia katika ukusanyaji, usafirishaji hadi utunzaji wake katika madampo ya kisasa matatu yanatarajiwa kujengwa chini ya mradi huu," amesema Mchengerwa.

Kadhalika, amesema kupitia mradi  huo master plan ya mifereji mikubwa ya maji ya mvua itaboreshwa na mifereji muhimu itatambuliwa na itajengewa yenye jumla ya kilometa 90 kwa Dar es Salaam nzima.

"Mradi huu ni ishara kuwa Serikali ina nia thabiti ya kutatua changamoto za miundombinu ya Dar es Salaam na kubadilisha hali ya Jiji letu," amesisitiza Mchengerwa.

Naye, Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema  mradi huo utatakelezwa kwa muda wa miaka sita kuanzia mwaka 2024/25 na gharama yake ni EURO milioni 361.1 sawa na sh. bilioni 988.083 zitaleta mabadiliko chanya makubwa katika Jiji  la Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkaaza wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesema ni fahari kwao kushiriki katika kukuza na kuendeleza Jiji la Dar es salaam, kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita Benki ya Dunia imetoa zaidi ya Dola bilioni  1.5 kwa ajili ya uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.

Benki ya Dunia kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI wamekwishatoa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua changamoto za miji ya Tanzania hasa katika kuboresha miundombinu muhimu ya mijini ikiwamo mradi wa ULGSP, TSCP pamoja na DMDP awamu ya kwanza na kwa sasa  wametoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa  mradi wa TACTIC katika miji 45 nchini.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA

    June 15, 2025
  • MANYARA BINGWA RIADHA WASICHANA NA WAVULANA MITA 1,500

    June 15, 2025
  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.