Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

DKT.MAGEMBE ATOA MAELEKEZO 11 KWA SEKRETARIETI ZA MIKOA NA HALMASHAURI

Imewekwa tar.: July 7th, 2022

Serikali  imetoa maelekezo 11 kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu za Mipango, Uratibu na Serikali za Mitaa, Maafisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji na Waweka Hazina wa Halmashauri wanayopaswa kuyatekeleza kwa tija na ubunifu ikiwemo la kusimamia mpango ya bajeti na kuongeza uwajibikaji wa pamoja.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 7 Juni, 2022 Jijini Dodoma na Naibu Katibu Ofisi ya Rais ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt.  Grace Magembe (afya) aliyemwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikai za Mitaa, Innocent Bashungwa wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili kwa maafisa hao.

Amesema kuna haja ya kuwa na uwajibikaji wa pamoja kwa watumishi wa Mikoa na Halmashauri sambamba na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/23.

“ Mikoa na Halmashauri ni taasisi ambazo kila kinachofanyika lazima kila mmoja ahakikishe amefanya kwa nafasi yake badala ya kuja na visingizio mimi sijui, mimi sikuhusika maana mwisho wa siku wote tutawajibika kwa utendaji mzuri au mbaya wa taasisi.” Amesisitiza Dkt. Magembe

Amewahimiza kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma ikiwamo zile za mapato ya ndani ya halmashauri ili ziweze kutekeleza miradi iliyopangwa na Serikali .

“ Niendelee kukemea matumizi ya fedha mbichi na niwatake kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuchukua hatua kwa wakati kwa watendaji watakaoshindwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma na zile za taaluma zao.” amesema Dkt. Magembe

Pia awamataka maafisa hao kuhakikisha wanasimamia umalizaji wa miradi kwa wakati na viwango na kuwa serikali haitavumilia kuona kuna miradi viporo. Aidha, amewataka kusimamia na kuratibu upelekezaji wa asilimia 40 au 60 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwenye miradi ya maendeleo.  

Dkt Magembe amewaeleza kuwa kuanzia sasa utendaji wa sekretariati za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa pamoja na mambo mengine utapimwa kwa vigezo vya upelekaji wa fedha za miradi asilimia 40 kwa 60 kwenye miradi ya maendeleo,pia  kuhakikisha wanasimamia  upelekaji, matumizi na urejeshwaji wa wa fedha za mikopo ya asilimia 10

Pia amesisitiza suala la matumizi na usimamizi wa mifumo ya ndani ya udhibiti wa makusanyo na matumizi ya fedha ili kuhakikisha hoja za ukaguzi zisijitokeze na kuhakikisha hoja za zamani zinajibiwa na kufungwa.

“ Hili suala la kutozalisha hoja mpya za ukaguzi na kuzimaliza zilizoibukwa pia kitatumika kama kigezo cha utendaji wenu hivyo tuache visingizio.”

Maofisa hao pia wametakiwa kusimamia uandaaji wa Taarifa ya Mwisho ya Hesabu za fedha Mamlaka za Serikali za mitaa kwa wakati na kwa usahihi na kusimamia usluhisho wa kifedha unafanyika kila mwisho wa mwezi kwa kuzingatia memoranda ya fedha za Serikali za mitaa ya mwaka 2009.

“ Hakikisheni  mnafuatilia   mara kwa mara wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo katika Mikoa unafanyia ili kuwa na thamani ya fedha kama ilivyokusudiwa.” amesisitiza

Aidha,  amekumbusha kuwasilisha maombi ya fedha za miradi ya maendeleo kupitia ruzuku ya Serikali kuu mapema ili kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyopangwa utekeleaji kuanza mapema.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.