Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Msonde aagiza mafunzo ya mfumo wa NeST

Imewekwa tar.: March 5th, 2024

OR - TAMISEMI

MAKATIBU Tawala wa Mikoa nchini wametakiwa kuhakikisha wakuu wa shule za msingi na sekondari na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya wanapewa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi (NeST) kabla ya kuanza kutumika.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa itaongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi hasa ikizingatia kuwa Serikali inakusudia kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde wakati wa kufungua mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa umma (NeST) yanayofanyika katika Ukumbi wa shule ya msingi Mtemi Mazengo Jijini Dodoma.

Alisema Serikali imekuwa ikipeleka fedha nyingi za kutekeleza miradi katika ngazi ya mzingi hivyo Ma-RAS, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara ya halmashauri kuhakikisha wanafundisha kwa ukamilifu wale wote wanaotekeleza shughuli za manunuzi katika ngazi ya msingi wakiwemo wakuu wa shule na waganga wafawidhi.

“Mkifanya hivyo shughuli za manunuzi zitakwenda vizuri, thamani ya fedha itaonekana kwenye miradi na itakamilika kama vile ambavyo serikali inataka.”

Pia amewataka wataalamu wote watakaohusika katika mchakato wa manunuzi kuhakikisha wanazingatia matumizi ya mfumo huo ili kujiepusha na makosa ambayo yanaweza kuwatia matatani.

Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa ya kuhakikisha wataalamu katika serikali za mitaa wanatumia mfumo wa manunuzi wakati wa kutekeleza miradi ya ujenzi katika maeneo yao.

“Ukiwa hapa usijadili kama mtu wa Dodoma bali mwakilishe wengine ambao hawako hapa kutoka mikoa yote ya Tanzania, hivyo mnapopewa mafunzo haya myasikilize vizuri na myaelewe, palipo na utata mseme ili msije kupitisha vitu ambavyo kiuhalisia havitekelezeki,” amesema Dkt. Msonde wakati wa kusisitiza umakini wa washiriki wa mafunzo hayo.

Awali, Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Erick Kitali amesema idara yake itaendelea kuwekeza katika kuboresha na kubuni mifumo ambayo ni rafiki kwa matumizi kwa manufaa ya serikali na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake meneja wa mafunzo na huduma za ushauri kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Castor Komba amesema imehakikisha inaboresha mfumo wa ununuzi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza leo (Machi 4, 2024), yanashirikisha washiriki 45 ambao ni waganga wafawidhi, makatibu wa afya, maafisa ununuzi wa mikoa na halmashauri, wakuu wa shule na walimu kutoka katika halmashauri tatu za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Bahi, Chamwino na Dodoma jiji.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.