Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Gwajima aweka reheni Vyeo vya Watumishi Makole.

Imewekwa tar.: November 2nd, 2019

Baadhi ya watumishi wa Afya katika Kituo cha Afya Makore mkoani Dodoma wamejikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na taratibu zinavyo elekeza. Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Daktari Dorothy Gwajima amesema, kutokana na kukithiri kwa utendaji wa mazoea kwa baadhi ya watumishi wanaopima upepo sasa kaguzi zote zitaanza kufanyika kwa mwelekeo wa kutathmini jinsi gani kila mtumishi wa kada husika ametekeleza majukumu yake kama yalivyoelekezwa kwenye muundo wake wa utumishi.

Aidha, amewaeleza watumishi hao kuwa, inaonekana maboresho yanayoonekana katika kituo hicho yakawa yanafanywa na watumishi wachache wanaofidia utegaji wa wengi hivyo, kutokana na mwenendo huo sasa hatasita kuwashtaki wazembe wote kwa Katibu Mkuu utumishi ili hii habari ya kupandishana vyeo iende sambamba na chujio makini la ufanisi wa kila mtumishi na kiongozi mahala pa kazi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ufuatiliaji endelevu unaofanywa na Naibu Katibu Mkuu na jopo la wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI katika kituo hicho na vingine nchini ambapo, kituo cha afya Makore ni mojawapo ya vituo vinavyojengewa uwezo viwe vya mfano katika mabadiliko ya mifumo ya uwajibikaji mahala pa kazi. Mwelekeo huu ni utekelezaji wa mojawapoa ya Azimio la Kikao cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kilichofanyika Agosti, 2019 kuwa, kila halmashauri iteue vituo 4 vya mfano.

 “Sitasita kumshauri Katibu Mkuu Utumishi asiridhie baadhi ya watumishi miongoni mwa 80 mnaowaombea wapandishwe vyeo iwapo nitabaini ufanisi wao hautoshi kupitia kaguzi tunazofanya. Nitamwambia Katibu Mkuu hawa watumishi hawastahili kupanda vyeo kwakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo na hapa msisingizie eti mko wachache wakati idadi yenu ni mara mbili ya wanaotakiwa hapa,” alisema Gwajima na kusisitiza kuwa,“haiwezekani zaidi ya miezi mitatu wataalamu wa kitengo cha dawa eti hawajahuisha taarifa za dawa kwenye kitabu husika (Ledger) yaani mnajifanyia fanyia tuu bila utaratibu halafu mnasema dawa hazitoshi huku mmeotesha vichaka vyenye utata wa kujua wapi mmezitumia?” alihoji Gwajima.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu pia, alifanya uhakiki wa hadi ujazo wa kila kitendanishi cha maabara kwamba kilitakiwa kupima sampuli ngapi na mwisho kimepima ngapi ambapo, alibaini wataalamu wa maabara wamepima sampuli nyingi zaidi kuliko walizotakiwa kupima huku wakiwa hawana kumbukumbu za kiofisi kuhusu wapi walikopata vitendanishi vya ziada, ‘inakuwaje ulitakiwa kwa kitendanishi hiki upime sampuli 50 badala yake umepima 350”? Gwajima alihoji.

Naye mtaalamu wa Maabara katika kituo hicho Ndugu Godfrey Mahundi hakuwa na majibu yakina juu ya wapi hasa alitoa ziada hiyo ya vitendanishi na kama ipo sehemu alikotoa kwa nini hakuna rekodi ya aliyempa wala yeye kukiri mapokezi.

Dkt. Gwajima alisema, kwa kawaida taratibu za uchukuaji dawa lazima ziwe zinaandikishwa kutoka eneo moja hadi lingine yaani kutoka hifadhi kuu, hifadhi ya kati, hifadhi ndogo mpaka zinapomfikia mgonjwa na hata kama amepewa toka kwenye kituo kingine lazima kuwe na rekodi za aliyetoa na aliyepokea.

“Hapa Kituo cha Afya Makore baadhi ya watumishi wameelewa somo hasa eneo la huduma za kitabibu na kiuguzi ila nyie watu wa maabara na dawa ndiyo bado mnapima upepo mnajifanyia mambo kienyeji kwa kutoandika kumbukumbu za matumizi ya raslimali za dawa na vitendanishi na nani katumia, nasema nyie pamoja na wengine wote nchi nzima wanaofanya mambo kama yenu ambayo, yanayoruhusu kushamiri kwa vichaka vya matumizi mabaya ya raslimali za vituo sasa wakati umefika wa kuamua kurudi kwenye mstari ama mtausikia tu utumishi wa umma kwenye redio. Aliendelea kusisitiza Katibu Mkuu.

Amesema kituo hicho ni cha mfano na watakaofanya hapa lazima wawe wa mfano na si vinginevyo, huwezi kuwa mtumishi wa kituo cha mfano huku wakitoa fursa ya majizi kujificha kwenye kazi zao. Ameongeza kuwa ijulikane kuwa hizo  ni salamu zake kwa vituo vyote vya afya nchini.

Katika hatua nyingine Watumishi hao walionesha kutambua uzembe walioufanya na kukiri kuzembea katika utendaji wao huku wakiomba msamaha na kuahidi kubadilika.

Akikiri kufanya uzembe Mfamasia wa Jiji la Dodoma George Hondi, kwa niaba ya watumishi wengine, alisema wanaona fedheha na aibu kwani yote yaliyobainishwa na Naibu Katibu Mkuu hakuna hata moja la kusingiziwa wala kuonewa.

“Ni kweli hatujatekeleza na kusimamia majukumu yetu na hili ni kosa na sisi tuseme tu na kunaahidi kubadilika” alisema Hondi.

Kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 1 wa Mwaka 2009 unaoeleza juu ya Miundo ya Utumishi kwa Kada za Afya chini ya Wizara ya Afya yapo mambo mengi ambayo yameendelea kugundulika kupitia ziara hii na zingine za Naibu Katibu Mkuu na timu yake na yanayotokana na baadhi ya watumishi kujifanyia kazi kienyeji mfano, Mfamasia Daraja la Pili anayo majukumu yake ikiwemo kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba na kutekeleza maelekezo ya wizara kuhusu ufanisi wa Kamati ya Dawa kwenye kituo husika lakini wengi hawafanyi na sababu hawana lakini wanadai wapandishwe vyeo Hii haiwezekani” amesema Dkt Gwajima.  .

Chini ya OR-TAMISEMI imeundwa timu rasmi ya kuwa inafanya ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu ya kila mmoja tutajua huko huko wapi hawatoshi na wapi wako idadi kubwa lakini hawana tija.

Dkt. Gwajima amewataka Makatibu wa Afya kutokuwa makarani wa kuorodhesha tu majina ya watu kupanda vyeo kisa mtumishi kaajiriwa siku nyingi bali wapime ufanisi ili kumtendea haki anayejituma na mzembe naye apate haki yake ya kutopandishwa cheo au kushushwa. Amesema wataimarisha mifumo na taratibu za kujipima na kuwapima watumishi ili haki itendeke haraka kwa wale wanaojituma na wasiojituma pia wapate haki yao mapema tu kila mtu abebe mzigo wake.

Mapema juma lililopita, Naibu Katibu Mkuu akifungua Kikao cha Wafamasia wa Mikoa mjini Dodoma, aliwarushia lawama wataalam wa Afya hususani kada ya Famasia kwamba, wizi wa dawa unaoshamiri unachangiwa na usimamizi mbovu eneo lao kiasi kwamba dawa hizo zinapotea bila taarifa kwa kuwa hawazingatii au kwa makusudi wanafanya kazi huku wakitoa fursa nzuri kwa wezi na wadokozi kutekeleza azma yao na hii ni kusaliti juhudi za Serikali za kuongeza bajeti ya dawa na kufikia bilioni 269, hivyo akaapa kupambana nao kwa kuomba nguvu za wananchi kuwafichua wote watakaobainika kuhujumu jitihada hizo.

Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa mujibu Muongozo wa sasa ndio msimamizi Mkuu wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati kote nchini.

Baadhi ya watumishi kituo cha Afya Makore wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu.

Mfamasia akiingiza dawa katika kitabu cha kumbukumbu za dawa, Kituo cha Afya Makore


Na. Atley Kuni- TAMISEMI.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.