Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Gwajima atumia saa 2:56 kuwakumbusha timu za Afya Singida majukumu yao ya Msingi.

Imewekwa tar.: January 28th, 2020

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima, ametumia saa 2 na dakika 56 kuwafunda na kuwakumbusha watumishi wa kada ya afya juu ya majukumu yao ya msingi na kuwahimiza kuyafuata kwa kuyawekea mipango halisi.

Dkt. Gwajima amefanya hayo mwishoni mwa juma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida alipokutana na timu za uratibu Afya za Wilaya zote za Mkoa huo wakiongozwa na timu ya Afya ya Mkoa.

Akitoa somo katika kikaokazi hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Angelina Lutambi, Dkt. Gwajima alisema, changamoto kubwa inayowakabili watumishi wengi ni kushindwa kupanga mpango mzuri wa kutekeleza kikamilifu majukumu yao ya ajira kwa vigezo stahiki. Alisema,  utekelezaji unaofanyika nikwa mazoea lakini  sio kwakufuata uhalisia kwa takwimu bayana.

Aliwataka Viongozi na waratibu hao wa afya kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa majukumu kwa kuhakikisha kwanza kila mtumishi amepewa majukumu yake na kueleweshwa ipasavyo, kisha kuongozwa kwa kuandaa mpango kazi wake wenye vigezo na siyo jumla jumla tu kwani bila kufanya hivyo watumishi wengi hujikuta wanatekeleza majukumu ya mazoea na kwa mifumo ya mazoea.

Kuhusu suala la majukumu yanayohusu utawala wa masuala ya afya Dkt Gwajima alisema, hilo ni suala mtambuka linalohusu wataalamu wengi wakiwemo maafisa utumishi, maafisa manunuzi, wakaguzi wa ndani, waajiri na wengine kutoka idara mbalimbali zisizoangukia sekta ya afya kitaaluma. Dkt. Gwajima alisema iwapo wataalamu hawa hawatawajibika kikamilifu na kwa wakati basi nao wanaweza kuchangia ufanisi wa utekelezaji majukumu ya afya kushuka viwango.

Akitoa mfano wa uhusiano wa Idara zisizo za taaluma ya sekta ya afya alisema “je dokezo la kuomba utekelezaji wa shughuli za afya huchukua muda gani kufanyiwa kazi na afisa manunuzi, afisa utumishi, afisa fedha na wataalamu wengine?" Alihoji Dkt. Gwajima.

Jinsi gani Afisa Utumishi anaona umuhimu wa kuchambua uwingi wa kazi baina ya watumishi na kuwafanyia mgawanyo upya? Au Mkaguzi wa ndani anasimamia vipi masula ya ukaguzi wa stoo zetu za mali mbalimbali iwapo mifumo ikp vizuri ikiwemo dawa na uwepo wa kumbukumbu za mali zilizopo kwenye vituo kwa ujumla?” alizidi kuhoji Dkt. Gwajima.

Aidha alisema, katika hili la utawala lazima kila mtu kwa nafasi yake asimame kidete ili sekta hii inayochangia katika safari ya kwenda uchumi wa kati iweze kuwa ma utayari wakati wote katika kuhakikisha abiria wote wako katika afya njema kwa ajili ya kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Angelina Lutambi, alisema tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni kwa baadhi ya watumishi kutokuwa na ubunifu wa maarifa na kufanya kazi kwa mazoea.

“Utakuta mtu ni Mkuu wa Idara lakini ukimuuliza umetelekeza majukumu gani hajui, anakwambia hujanipatia jambo la kufanyia kazi, wakati mtu huyo ana muongozo wa majukumu yake.” Alisema Dkt. Lutambi na kuongeza kuwa, kuanzia sasa atayasimamia yote ambayo Naibu Katibu Mkuu amewaelekeza watendaji wa mkoa huo  na kwamba, hata yeye tayari alishaona hizo changamoto na sasa atahitaji kupata taarifa ya kila wiki kupitia kwa Mganga Mkuu wa Mkoa kuhusu muelekeo wa masuala ya Afya katika Mkoa.

Kwa upande wake Mlezi wa Mkoa wa Singida katika masuala ya afya, kutoka OR-TAMISEMI, Bibi Mary Shedrack alisema, ili sekta iweze kufanikiwa lazima kuzingatia vigezo vitakavyo waongoza kwa kila mmoja kuvitatumika na kupima kwa kila robo.

Ziara ya Dkt. Dorothy Gwajima ni muendelezo wa ziara za kikazi anazo zifanya katika kufatilia masuala mbali mbali ya afya nchini na katika ziara hii imemchukua siku mbili katika Mkoa wa Singida kwa ajili yakufatilia hali ya utoaji huduma za afya na vilelvile kuzungumza na timu za uratibu za afya za Wilaya za Mkoa huo.  

Na. Atley Kuni- SINGIDA.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.

    May 24, 2025
  • SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI

    May 24, 2025
  • DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.

    May 24, 2025
  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.