• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Dkt. Gwajima aja na mwarobaini wa upotevu wa dawa nchini

Imewekwa tar.: August 12th, 2020

Serikali  imeiagiza Mikoa yote nchini kufanya ukaguzi mara moja katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi ili kujua mfumo na mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba ,vitendanishi na kuchukua hatua stahiki zikiwemo za kuziba mianya ya wizi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima  katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.

Dkt. Gwajima ameeleza kuwa kuna baadhi ya watu wamegeuza Serikali kuwa shamba la bibi kwamba kila mtu atafanya anavyojisikia huku watanzania wanyonge wakitaabika kwa kukosa dawa wanapokwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

“Naagiza  uchunguzi huo ufanyike ndani ya miezi mitatu na kuleta taarifa ifikapo 15 Oktoba, 2020 ili kujua nini kinaendelea katika vituo vyetu, hatua gani zimechukuliwa ngazi ya Halmashauri na Mkoa na zipi zichukuliwe ngazi ya kitaifa kulingana na matokeo ya zoezi hilo”, ameelekeza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema kuwa, sharti ukaguzi huo ufanywe na wataalamu wa ukaguzi na uchunguzi yaani wakaguzi wa ndani (CIA) mkoa, halmashauri na maafisa ugani wa ngazi husika kama ilivyofanyika hapa Simiyu.

Amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kutoa ushirikiano stahiki kwa timu hizi za ukaguzi ili kuweza kukamilisha zoezi hilo kakamilifu.

“Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri muwawezeshe Wataalamu na Wakaguzi. Wakuu wa Mikoa na Wilaya fuatilieni utekelezaji kama ambavyo Mhe Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alivyokuwa mstari wa mbele kushirikiana na Katibu Tawala wake na sasa wameona matunda kuwa kumbe inawezekana dawa, vifaa tiba na huduma za vipimo kuwepo na vituo vikaongeza mapato ya uchangiaji hadi zaidi ya mara 4 ndani ya miezi sita tu, Simiyu wamethubutu, wameweza na wameiona tija hivyo wengine chukueni hatua kwa kujifunza toka kwao”, Amesisitiza Dkt Gwajima.

Pia Dkt. Gwajima amebainisha  kuwa katika fedha na mali yoyote ya Serikali hakuna mchezo wa mzaha hivyo kila mtumishi mwenye dhamana ya kusimamia anao wajibu wa kutoa taarifa ya matumizi.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amesema kuwa ni lazima yapatikane mapinduzi makubwa na ya haraka katika kutunza rasilimali za afya, haiwezekani Serikali itoe mtaji mkubwa wa raslimali dawa, vifaa tiba na vitendanishi, mishahara, majengo, ilipe umeme na maji halafu kuwa tegemezi  wakati  takwimu za ukaguzi wa awali hapa Simiyu zinakiri kuwa inawezekana kupunguza utegemezi.

Ameitaja mikoa iliyofanya vizuri  katika kutekeleza  agizo la Ofisi ya Rais TAMISEMI  la utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya kuwa ni Morogoro, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Arusha.

“Nawaagiza ukaguzi huo uwe endelevu na usiwe ukaguzi wa macho bali wa vitendo kwa takwimu sahihi zenye ukweli ili wachezea mali ya umma wauone ukweli kwa macho na masikio yao kuwa hatuna mchezo na hatuonei mtu ni kweli mtupu na wao ni mashahidi”, ameagiza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amelekeza kuwa lazima kila mkoa na halmashauri uhakikishe vituo vyote vina vitendea kazi vya utunzaji mali ya umma vikiwemo leja za mali, vitabu vya kuombea na kutolea mali toka stoo (requisition and issue vouchers), kadi za kufuatilia rekodi za mali inayotoka (bin cards), risiti za dawa (prescriptions), fomu namba 2C ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na watumiaji wa vifaa hivyo wanafundishwa na kuelewa na kumiliki na kutumia na kufanyiwa ufuatiliaji wa utumiaji.

Hata hivyo, Dkt. Gwajima amesema ipo mifumo mbalimbali ya kiteknolojia (TEHAMA) ambayo inatunza kumbukumbu za raslimali za afya mfano ELMIS lakini ajabu ni kuwa Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Ugani hawajawezeshwa kuifahamu na kupewa Nywila (Password) ili wawe huru kuingia na kufuatilia ikiwemo kukagua.

Dkt. Gwajima ametoa wito wa kufungwa mfumo wa GOTHOMIS utakaosaidia  katika shughuli zao za kiutendaji na kwa ufasaha, hivyo mfumo huo  ufungwe na kila mwezi  kuwepo na taarifa  ya hatua zinazoendelea  na asiyefuata maagizo  haya atahitaji kufanyiwa ukaguzi maalum.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemuagiza  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Miriam Mbaga kuunda kikosi kazi kitakachofanya uchunguzi juu ya upotevu wa dawa katika halmashauri zote zilizoko katika Mkoa huo na kuja na taarifa ya kilicopatikana katika ukaguzi huo.

Na.Majid Abdulkarim, Simiyu

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.