Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Biteko azindua Namba 115 Mfumo wa M-Mama

Imewekwa tar.: March 26th, 2024

Na Fred Kibano, Dodoma

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amezindua namba 115 kama suluhisho kwa dharura za wajawazito waliojifungua na Watoto wachanga nchini Tanzania.

Dkt. Doto Biteko amezindua namba hiyo leo tarehe 25 Machi, 2024 baada ya kutoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa afyamsingi Jijini Dodoma na kusema mfumo huyo sasa upo nchi nzima na kila mtanzania akina mama na akina baba wanaweza kuutumia kuokoa maisha ya mama wajawazito na Watoto wachanga. 

“Mfumo wa usafiri wa mama wajawazito, waliojifungua na Watoto wachanga M-Mama umefika nchi nzima, akina mama 2,370,000 wanajifungua na kati ya hao akina mama 75,000 wanapata dharura zinazohitaji usafiri wa kuwapeleka kwenye vituo vinavyotoa huduma stahili kutokana na huduma ya kutaka kujifungua” alisema Mhe. Biteko.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (AFYA) Mhe. Dkt Festo Dugange alisema hadi kufikia mwezi Februari, 2024 huduma za afyamsingi nchini vipo vituo vya kutolea huduma za afya 6,933 ambapo zahanati 5,887 vituo vya afya 874 na hospitali za halmashauri 172 ikiwa ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watanzania 

Kuhusu utoaji wa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na wagonjwa waliolazwa (IPD) kwa mwaka 2023 wagonjwa waliopata huduma walikuwa milioni 26.9 walipata huduma katika vituo vya afyamsingi (OPD) na wagonjwa waliolazwa (IPD) walikuwa 854,318 wakati huduma ya mama na mtoto jumla ya wateja milioni 1.6 walijifungulia katika vituo vya kutolea huduma afya msingi na wakina mama 125,318 waliokuwa na uzazi pingamizi walifanyiwa upasuaji.

Kwa upande wake Agapinus Tax akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania ambaye ndiye mdhamini wa Mfumo wa M-Mama amesema mwaka 2022ulifanyika uzinduzi wa Mfumo wa M-Mama kwa lengo la kuwafikia wananchi wote nchini na sasa mfumo upo nchi nzima na kwamba hiyo ni chachu ya kuwa na jamii yenye afya bora na kusisitiza kwa pamoja tunaweza.

Naye Mkurugenzi wa M-Mama Tanzania Dolorosa Duncan kutoka Pathfinder International Tanzania  amesema namba ya huduma ya dharura ya 115 ni kwa ajili ya kina mama wajawazito na waliojifungua chini ya siku 42 na watoto wachanga wenye dharura na sio akina mama waliopatwa na uchungu wa kujifungua. 

Mkurugenzi Dolorosa ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Sekta binafsi na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidi zaidi ili mfumo huo umfikie mama mjamzito akiwa nyumbani

"kwa sasa huduma hii ya Simu ya dharura inatolewa kwa ngazi ya kituo kimoja cha afya na kingine nchi nzima ila kwa mkoa wa Shinyanga huduma hii ya dharura imefika mpaka ngazi ya jamii na sasa tunaongeza mikoa mitano ya Tanzania Bara na mkoa mmoja wa Tanzania Visiwani na malengo yetu ni kufika katika mikoa yote Tanzania," alisema Mkurugenzi Dolorosa Duncan.

Itakumbukwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua Mfumo wa M-Mama tarehe 6 Aprili, 2023 Jijini Dodoma ili kila mama mjamzito, aliyejifungua na mtoto mchanga waweze kupata huduma kwa wakati na kuokoa Maisha na sasa uzinduzi wa namba 115 unaonyesha Serikali ya Awamu ya Sita imejitoa katika kuboresha mifumo ya kukabiliana na dharura, kukuza mustakabalisalama na wenye afya kwa watanzania wote.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.