Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dawa muhimu kupatiwa ufumbuzi Vituo vya Afya, Hospitali – Dkt. Mpango

Imewekwa tar.: July 22nd, 2022

Na Fred kibano Mpanda Katavi

Serikali imesema imejipanga kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana katika Vituo vya Afya na hospitali mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akiongea baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Nsemulwa Mpanda Manispaa hapo jana Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema suala la dawa linaendelea kupatiwa ufumbuzi ambapo mpaka upatikanaji wake ni asilimia 90 katika vituo vya afya na hospitali.

“serikali imejipanga kusogeza miundombinu ya huduma mbalimbali ya afya,elimu, maji kwa wananchi tunaendelea kuhakikisha jitihada ya dawa muhimu zinapatikana katika vituo vyetu vya afya na hosptali mbalimbali na hivi sasa upatikanaji wa dawa ni asilimia 90” alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Philip Mpango amesema kukamilika kwa kituo hicho kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kutasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya na ile ya rufaa kwa kuwa huduma zote za msingi zitatolewa katika kituo cha afya Nsemulwa.

Amewaasa wazazi kuzingatia masuala ya lishe bora kwa watoto kwani lishe duni inasababisha kuzaliwa kwa watoto ambao hawana uwezo mkubwa wa kufikiri na hili litaepukika kwa kuzingatia lishe bora kwa kuwa mkoa wa Katavi unazalisha chakula kingi mpaka ziada ya kuuza nje ya mkoa na nje ya nchi ya Tanzania.

Katika hatua nyingine Dkt. Philip Mpango amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuacha kuwatoza wananchi ushuru wa mazao chini ya tani moja kwa kuwa Serikali ilikwishatoa agizo hilo la kuacha kuwatoza wakulima ikiwa ni pamoja na kujenga barabara ya lami kutoka katikati ya Mji wa Mpanda hadi kituo cha Afya Nsemulwa ambayo ni umbali wa zaidi ya kilomita moja ili kuondoa adha kwa wagonjwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema katika kuboresha Sekta ya Afya mkoani Katavi magari mawili ya wagonjwa yaliletwa, mashine nne za mionzi zimeletwa ambapo moja itakuwa Manispaa ya Mpanda lakini pia Serikali imeondoa ada kidato cha tano na sita ili kuwapa nafuu wananchi.

Akisoma taarifa ya Kituo cha Afya cha Nsemulwa Dkt. Paul Swakala Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda amesema kuwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri kiasi cha shilingi milioni 336 yalipokelewa na kutumika ambapo mpaka sasa maabara, vyoo na jengo la wagonjwa wa nje limekamilika na majengo mengine yapo katika hatua mbalimbali.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mlindoko amesema jumla ya vituo vitatu vinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ambavyo ni pamoja na Kituo cha Afya Nsemulwa Mpanda Manispaa, Halamashauri za Mpimbwe na Tanganyika ambavyo kila kimoja kitagharimu shilingi milioni 500 na ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamillah Yusuph amesema Wilaya yake ilipokea jumla ya shilingi Bilioni 33.03 kwa ajili ya kutekeleza miradi yote ya maendeleo kwenye Wilaya yake lakini pia fedha zilizojenga kituo cha Afya Nsemulwa zimetokana na mapato ya ndani na sio fedha za Serikali Kuu hivyo hii ni dalili ya kuanza kujitegemea.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.