Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Bilioni 33.5 zatengwa kwa ajili ya ujenzi wa wodi Hospitali za Wilaya 67 nchini

Imewekwa tar.: September 9th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa SERIKALI imetenga jumla ya Sh bilioni 33.5 kwa ajili ya kujenga wodi katika hospitali 67 mpya za Wilaya zinaoendelea kujengwa.

Ameyasema hayo leo akiwa kwenye ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo ya ujenzi hospitali ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa katika kijiji cha Mlowa Barabarani, Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kuwa baada ya Serikali kukamilisha ujenzi wa majengo saba katika awamu ya kwanza, pia inatoa Sh milioni 500 kwa kwa Hospitali 67 zilizojengwa katika kila Halmashauri nchini ili kuongezea majengo hayo.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli ametoa shilingi milioni 500 kwa kila hospitali za wilaya zilizojengwa  ili zitumike kujenga wodi za kulaza wagonjwa lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya  na kuwawezesha wananchi kupata huduma bora” Amesema Mhe. Jafo  

Mhe Jafo amesisistiza kuwa hatatoa fedha  hizo mpaka atakapohakikisha ujenzi wa majengo saba yanakamilika kwa asilimia 100 kwa kuwa zikitolewa mapema zitatumika kwa matumizi mengine jambo ambalo litakuwa ni kinyume na malengo yaliyopangwa

Kuhusu Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino Mhe Jafo amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa  na kuwahamasisha kuhakikisha wanakamilisha baadhi ya vitu vilivyobaki ili wananchi waweze kupata huduma.

"Hapa mlipofikia nimeridhishwa ingawa mmechelewa, hali mliyokuwa nayo nilipokuja awali ilikuwa mbaya na ya aibu, tusingesimamia kwa karibu mpaka sasa kungekuwa hakuna kitu.”Amesema Mhe. Jafo

 Mhe.  Jafo ameagiza mhadisi mshauri kuhakikisha anasisimamia kwa karibu umaliziaji wa hospitali hiyo ili kusiwe na kasoro ambazo zinaweza kuharibu kazi nzuri iliyofanyika.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge pamoja na kuishukuru serikali kuhakikisha huduma za afya zinaimarika katika Mkoa wa Dodoma, amesema Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linatarajia kuingiza umeme katika majengo hayo kuanzia wiki ijayo.

"Mkandarasi aliyepewa kazi ya kufikisha umeme wa REA ndiye atakayeingiza umeme kwenye majengo yetu haya na kazi hii inaanza wiki ijayo.”Amesema Mhe. Mahenge

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Chamwino, Athuman Masasi amesema wamepokea Sh bilioni 1.5 na mpaka sasa wametumia Sh bilioni 1.438 tangu kuanza ujenzi huo Februari mwaka huu  na kubakiwa na bakaa ya Sh milioni 61.

"Ujenzi wa majengo haya umefikia zaidi ya asilimia 80 na tuko katika hatua za umaliziaji. Tulishindwa kumaliza kwa wakati kwasababu mfumo wa malipo ulifungwa, lakini sasa zimefunguliwa baada ya kufanyika kwa usuluhishi wa kibenki, na ndio tunakamilisha yale yaliyobaki”. Amesema Masasi

Aidha amesema majengo yaliyokwishajengwa mpaka sasa ni Jengo la Wodi ya mama na mtoto, Jengo la Kufulia, Chumba cha Upasuaji, jengo la utawala, jengo la kuhifadhia maiti, chumba cha Mionzi na Jengo la kutolea dawa.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU  KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU 

    June 13, 2025
  • WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.