Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

BIL.22 KUJENGA SOKO NA STENDI USHIROMBO, BUKOMBE

Imewekwa tar.: July 29th, 2024

Na Angela Msimbira,GEITA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba  amesema  serikali imetenga  shilingi bilioni 22  kwa ajili ya ujenzi wa soko na stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Ushirombo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 15.8 zitatumika katika ujenzi wa soko  jipya la kisasa na Sh bilioni 6.26 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa stendi ambapo Serikali imetoa Sh bilioni 1 kama malipo ya awali ya utekelezani wa miradi hiyo inatarajia kuanza katika mwaka wa fedha 2024/25.

Akizungumza na wananchi wa Ushirombo leo Julai 28 ,2024 mkoani Geita, Mhe.Katimba amesema ujenzi wa somo hilo unaenda sambamba na mahitaji ya kipindi cha sasa.

Amesema soko la sasa uwezo wake vibanda vinavyoweza kubeba wafanyabishara 734 ambapo wenye vibanda halali ni 534 na wasio na vibanda ni 200.

Katimba amesema kuwa Serikali inawekeza Sh bilioni 15.89 kwenye ujenzi wa soko la kisasa litakalokuwa na mabanda kwa ajili ya kutosheleza wafanyabiashara 1,301.

"Ndugu zangu hii ni baraka kubwa sana kwa kuwa uwezo wa soko utaongezeka, wafanyabiashara wenye vibanda ambao kwa sasa wako 534 lakini soko likiboreshwa wataongezeka hadi kufikia wafanyabiashara 1,301."

Amesema kuwa uwekezaji huo mkubwa si kuwa utawanufaisha wafanyabiashara bali litasaidia kupata maeneo mazuri yakufanyia biashara inayokidhi kupata mitaji kwa wakati.

Katimba amesema kuwa kupitia ujenzi  huo wa soko la kisasa utasaidia ongezeko la mapato katika halmashauri ambapo awali halmashauri ilikuwa ikikusanya kiasi cha Sh milioni 51.3 kwa mwaka lakini soko likijengwa mapato yataongezeka hadi kufikia  shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka.

Amesema kwa upande wa mradi wa stendi eneo le  Ushirombo Katimba amesema kuwa kwa sasa stendi hiyo ina uwezo wa kupokea mabasi 50 kwa siku lakini baada ya kujengwa itakuwa na uwezo wa kupokea mabasi yasiyopungua 210 kwa siku.

Amesema pia ongezeko la mapato ni kutoka Sh milioni 155 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 1.4 kwa mwaka.

"Haya ni maendeleo makubwa yanayoenda kutokea ambayo yatasaidia kuboresha mapato ya halmashauri na jamii kwa ujumla ambapo yatasaidia kuboresha masuala mbalimbali ya maendeleo," amesema Mheshimiwa Katimba.

Amesema kuwe utekelezaji wa miradi hiyo kutasaidia pia ongezeko la ajira kwa wananchi wa Bukombe kwa kuwa miundombinu itaboreshwa ambapo serikali inatarajia ongezeko la ajira na kukidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati huu.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Geita hasa wafanyabiashara kupokea kwa moyo maendeleo makubwa yanayoenda kutokea katika eneo hilo kwa kuwa fedha zinazoenda kuwekezwa ni kubwa.

Amewataka  Halmashauri ya wilaya ya Bukombe kuhakikisha wakati wa utekelezaji wa mradi utumike utaratibu mzuri ambao hautakuwa kero kwa wafanyabiashara.

Amewataka kuhakikisha wafanyabiashara waliokuwepo awali wanapatiwa haki yao na kupewa kipaombele ya kuendelea kufanyabiashara kwenye eneo hilo

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe amesema kuwa Serikali imeridhia kiasi cha shilingi bilioni 1 kati ya 22 kwa ajli ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.

    May 24, 2025
  • SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI

    May 24, 2025
  • DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.

    May 24, 2025
  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.