Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Asasi za kiraia, Mashirika ya Kimataifa watakiwa kujenga miundombinu ya elimu nchini

Imewekwa tar.: July 26th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mwanza

Serikali imezitaka asasi za kiraia, taasisi za umma pamoja na mashirika ya kimataifa ambayo yanafanya kazi na serikali kwenye sekta ya elimu kuhakikisha kuwa yanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kujenga miundombinu ya elimu nchini kwa sababu ndiyo changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo hivi sasa.

Wito huo umetolewa jana katika kijiji cha Magaka wilayani Misungwi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda wakati akikagua mojawapo ya madarasa manne ya elimu ya  awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa na asasi ya kiraia ya TAHEA chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa kutoka nchini Scotland la Children in Cross fire katika wilaya za Misungwi na Ukerewe mkoani Mwanza.

Amesema kuanzia sasa asasi zote za kiraia na mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na masuala ya elimu mbali na kufanya kazi ya kufundisha na kujenga uwezo yatalazimika kujenga angalau darasa moja pamoja na matundu ya vyoo ili kuwezesha uwepo wa mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya awali nchini.

“Hatutakubali taasisi yoyote inayotaka kujihusisha na masuala ya elimu nchini kutumia raslimali kubwa katika maeneo ya  aina moja tu ya kujenga uwezo na kwenye masuala ya advocacy (ushawishi) na kuaacha kwenda kwenye matatizo ya kweli ambayo yanawakabili watoto, hasa haya maeneo ya watoto wa shule za awali,” amesema Naibu Katibu Mkuu na kuongeza:

“Kwasababu eneo hili bado hatujawekeza vya kutosha, kwa hiyo tunawataka wadau wote waje kutusaidia pale kwenye miradi mbalimbali inayohusiana na elimu ya awali kwa kutujengea angalau darasa moja kwa ajili ya choo na elimu ya awali.”

 Naibu Katibu Mkuu amesema kuwa serikali sasa imeazimia kuhakikisha kuwa watoto wote walio ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapata fursa ya kupata elimu ya awali, elimu ya msingi, na elimu ya sekondari bila ya vikwazo vyovyote.

Pia bwana Nzunda amewataka jamii na wazazi waendelee kuchangia elimu hasa katika maeneo ya chakula cha watoto wao wanapokuwa shuleni kama wanavyowajibika kuwapatia chakula watoto wao wanapokuwa majumbani kwao.

“Lengo ni kuwawezesha watoto wetu wawapo shuleni angalau wapate uji na chakula cha mchana ili waweze kusoma vizuri na kuchangamka wawapo madarasani," amesema.

Sambamba na hilo, jambo la pili ambalo Naibu katibu Mkuu amelisisitiza ni kuwataka jamii na wazazi kuisadia serikali kwenye miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali na wadau wa maendeleo kwa kuanza kujenga maboma kwa ajili ya watoto wanaosoma kwenye elimu ya awali,

Ameongeza kuwa kukamilika kwa maboma hayo kutawawezesha watoto wa elimu ya awali kuchangamka, wanajifunza mbinu za maisha, wanajenga mbinu za namna ya kuhusiana, wanajenga misingi ya utu, upendo, na furaha miongoni mwa watoto.

“Kwa kufanya hivi ninaamini tunaenda kujenga taifa la watoto wanaojitambua ambao wamejengewa misingi mizuri, tofauti na hao tutakuwa tunapoteza nchi na taifa,” amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Children in Crossfire bwana Craig Ferla alimweleza Naibu Katibu Mkuu kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na asasi ya kiraia ya TAHEA watajenga madarasa 100 ya aina hiyo katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pia ameelezea kufurahishwa kwake kwa jinsi uongozi wa juu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, mkoa wa Mwanza, halmashauri ya wilaya ya Misungwi, na kata za Mamae na Magaka kwa jinsi walivyompa ushirikiano katika kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo changamshi ya elimu ya awali katika wilaya ya Misungwi.

Bwana Craig amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa Children in Crossfire pamoja na TAHEA wana nia njema ya kujaribu kuchangia maendeleo ya Tanzania.

“Tunaamini kwamba hawa watoto wetu ambao ndiyo wako kwenye madarasa ya awali ndiyo taifa la kesho na tunaamini kuwa kama watapata mwanzo bora, wataweza kuchangia maendeleo ya taifa letu kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.