• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

ALAT 'Wafunguka' ushuru wa Majengo, Mabango na vitambulisho vya wajasiriamali

Imewekwa tar.: February 4th, 2021

Na Atley Kuni, DODOMA

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), imeipongeza Serikali kwa hatua yake ya kurejesha shughuli ya kukusanya kodi ya majengo, ushuru wa Mabango na vitambulisho vya wajasiriamali kwa Halmashauri kwani hatua hiyo itaongeza mapato kwa Serikali kutokana na mamlaka hizo kuwa na mtandao mpana wa kuvifikia vyanzo hivyo vya mapato.

Akizungumza Ofisini kwake leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa ALAT Taifa Bw. Elirehema Kaaya, amesema Jumuiya hiyo imefarijika sana kwa uamuzi huu wa Serikali kwani suala la kutaka vyanzo hivyo virejeshwe Halmashauri ilikuwa moja ya ajenda katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo, uliofanyika mwaka juzi, jijini Mwanza.

“Katika Mkutano Mkuu wa ALAT, uliofanyika kuanzia tarehe, 22 hadi 24, Julai, 2019, jijini Mwanza, moja ya ajenda ilikuwa kutazamwa upya kwa vyanzo vya mapato ili kushauri namna nzuri ya kuvirejesha katika Mamalaka ya Serikali za Mitaa, hivyo kwa hatua hii, Jumuiya ya Serikali za Mitaa tumefarijika sana, na kwakweli tunampongeza sana Mhe. Rais kwakutambua mtandao mpana wa mamlaka hizi, tunaimani kabisa watendaji katika mamlaka watajipanga na tija inayokusudiwa na serikali itapatikana” amesema Kaaya.

Ameongeza kuwa kutokana na mtandao wa Mamlaka za Serikali za Mitaa jinsi ulivyo, unaruhusu mamlaka hizo kutambua bango gani liko wapi, hivyo ni rahisi kwa watendaji wake kuweza kukusanya ushuru wake.

“Tunaposema Halmashauri zina mtandao mpana tunamaanisha kuwa mamlaka hizi zina uwezo wa kuwafikia wananchi wake kuanzia ngazi za wilaya, kata, vijiji au Mitaa hadi vitongoji hivyo siyo rahisi kuwepo suala la ukwepaji wa kodi, kwakuwa kwa umoja wao wanao uwezo wa kujipanga na kujua vichochoro vyote,” amesema.

Amesema Serikali ina wakusanya ushuru katika ngazi za kata, mpaka vijiji na hao wote waliwezeshwa mashine za kukusanyia mapato za POS, ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha suala la ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuzuia mianya ya ubadhilifu.

Katibu Mkuu huyo wa ALAT Taifa amekumbusha kuwa Mwaka 2019, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, iligawa mashine mpya za kisasa 7227 kwa mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuweza kusaidiana na mashine 10,100 zilizokuwepo awali, lengo likiwa ni kuzirahisishia Mamlaka hizo kukusanya mapato yake, mbalimbali

Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya fedha, tarehe 01 Februari, ilitangaza kurejeshwa kwa shughuli za ukusanyaji wa ushuru wa majengo, mabango na vitambulisho vya wajasiriamali katika mamlaka za Serikali za Mitaa, isipokuwa kwa vyanzo vilivyo chini ya TANROAD na TARURA,huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kuongeza mtandao wa kukusanya mapato hayo, ambayo yalikuwa yakikusanywa na Mamlaka ya mapato nchini. (TRA) toka ilipo kabidhiwa mwaka 2018.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.