logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

ZUIENI MIANYA INAYOASHIRIA UPOTEVU WA FEDHA – DKT. MFAUME.

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume  ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi .

Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni.

“ Tunapolenga upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi lazima tudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuongeza mapato kwa kutoa huduma bora Kwa wateja wetu” amesisitiza

Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT)  katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuongeza usimamizi wa fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.

Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) kushirikishana na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili kufanikisha utoaji wa huduma chanjo Kwa Watoto katika Halmashauri hiyo.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora