logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA RASMI UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 LEO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, leo Juni 9,2025 anatarajiwa kufungua rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari yanayofanyika  Kitaifa Mkoani Iringa.

Ufunguzi huo utafanyika katika viwanja vya michezo Kichangani Manispaa ya Iringa, na kuhudhuriwa na wanamichezo zaidi ya 3,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania, ambao tayari wameshawasili Mkoani humo.

Maandalizi ya zoezi hilo la ufunguzi yameshakamilika, likiwa lilitanguiiwa na ufunguzi wa Baraza la UMITASHUMTA lililofanyika jana tarehe 8 Juni 2025 katika viwanja vya shule ya Sekondari Lugalo-Iringa.

UMITASHUMTA & UMISSETA inaandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utamaduni na Michezo.

Kauli mbiu ya Mashindano ya mwaka huu ni "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu"

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora