logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Wauguzi imarisheni Usimamizi wa utoaji wa huduma bora za afya nchini - Dkt Dugange

Na OR-TAMISEMI, Dodoma  

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewaelekeza Wauguzi Viongozi wa ngazi zote za afya nchini  kuhakikisha wanaimarisha usimamizi wa utoaji wa huduma bora ili wananchi wote wapate huduma bora na kwa usawa

Dkt. Dugange ameyasema hayo leo Machi 27, 2025 wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa wauguzi viongozi uliofanyika katika ukumbi wa  Mikutano wa PSSSF  Jijini Dodoma wenye kauli mbiu ya inayosema HUDUMA BORA WAJIBU WANGU.

Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya sita imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hivyo  bila ya kuwepo kwa  huduma nzuri na bora kutoka kwa watoa huduma za afya, na hasa Wauguzi, uwekezaji huu hautakua na manufaa.

 

“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa  kwenye sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya, ununuzi wa vifaa na vifaa tiba, uboreshaji wa mazingira ya kazi, hivyo mapaswa kuwasimamia waliopo chini yenu ili wafanye kazi kwa weledi na uadilifu,” Dkt. Dungange amesisitiza.

Dkt. Dugange amewataka wauguzi wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni,  Taratibu, Miongozo na Miiko ya taaluma ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima katika eneo la utoaji wa huduma za afya msingi nchini.

“Tunatambua kuwa wauguzi wanafanya kazi nzuri sana japo kuna baadhi yenu wachache wanaharibu sifa nzuri ya wauguzi kwa kufanya makosa mbalimbali yanayoweza kuepukwa hivyo msisite kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wote watakaobainika kwenda kinyume, kukiuka maadili ya kitaaluma na kufanya ubadhirifu wa mali za umma, amesisitiza Dkt.Dugange

Aidha, amewataka  wauguzi hao kujiendeleza ili kupata wauguzi wenye ujuzi na maarifa zaidi ikiwa ni pamoja na Wauguzi Bingwa watakaosaidia kuimarisha upatikaji wa huduma za kibingwa katika hospitali zetu nchini.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora