logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

WATUMISHI KUJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA.

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume  amezielekeza timu ya usimamizi wa afya ya Mkoa wa Dar es Salaam (RHMT) na timu ya usimamizi wa afya (CHMT) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuandaa mpango kazi wa kuwajengea uwezo wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

Dkt. Mfaume amesema hayo kwenye kikao cha majumuisho katika hospitali ya Mbezi mara baada ziara yake yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kwenye Halmashauri hiyo.

“Imefungwa mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya lakini kufungwa tu haitoshi, tumeona kuna changamoto kubwa sana ya uwezo wa watumishi wetu kutumia mifumo hii hivyo Halmashauri iandae mpango kazi kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo” amesema Dkt.Mfaume

Amesema lazima halmashauri ziwekeze kwenye TEHEMA kwa kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwa  ni  muelekeo wa Dunia kwa sasa.

Aidha, Dkt. Mfaume amesema matumizi ya mifumo mbalimbali katika sekta ya afya yamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuboresha huduma na kuongeza mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora