logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Vituo vya kulele watoto vyabainika kuendeshwa bila kuwa na miongozo ya Serikali Kigoma.

OR - TAMISEMI

Serikali imetoa wito kwa wamiliki na waendeshaji wa vituo vya malezi na makuzi ya Watoto wadogo mchana kufuata taratibu,kanuni na miongozo ya uanzishwaji na uendeshaji wa vituo hivyo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazokidhi viwango ambavyo ni afya bora kwa Watoto,elimu ya awali, maelzi yenye mwitikio, lishe bora, ulinzi na usalama.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Ofisi ya Rais- TAMISEMI Shabani Muhali, baada ya kubaini baadhi ya vituo vya malezi na makuzi vya kuhudumia watoto wadogo mchana mkoani Kigoma kufanya shughuli za Malezi na Makuzo bila kuwa na miongozo ya serikali ya uanzishaji na uendeshaji wa vituo hivyo.

Akiongea kwa niaba ya timu maalumu ya tathmini na ufuatiliaji shughuli za malezi na makuzi Ofisi ya Rais - TAMISEMI  katika ziara maalumu  ya ufuatiliaji na tathimini  juu ya mwenendo wa utolewaji wa huduma za malezi na makuzi katika vituo hivyo, Shabani amesema timu hiyo imegundua mapungufu mengi ikiwa ni Pamoja na walezi kutokuwa na elimu sahihi ya malezi huku baadhi ya vituo vikiendeshwa bila mwongozo maalum maarufu kama kiongozi cha Mlezi.

Kufuatia hatua hiyo Shabani amesema maelekezo ya serikali ni kuhakikisha vituo vyote vya kutolea hudma za malezi na makuzi kwa Watoto wadogo mchna vinasajiliwa na kuendeshwa kwa kufuata miongozo maalum ili kutimiza dhamira njema ya uanzishwaji wa vituo hivyo.

Timu hiyo imekagua vituo mbalimbali vya kulelea watoto wadogo mchana katika wilaya za Kakonko  na Kasulu Mkoani Kigoma na inaendelea na ziara yake Mkoani Mbeya, ikiwa ni kufanya ufuatiliaji na tathmini, na pia kutoa ushauri chanya katika kuboresha huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura