logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA MAKANDARASI WA BARABARA WANAOJENGA CHINI YA KIWANGO

OR- TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI inataendelea kuwachukulia hatua wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa Barabara chini ya kiwango.

Hayo yamesemwa  leo Aprili 30, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Aleksia Kamguna,mbunge wa Viti maalum aliyetaka kujua serikali inawachukulia hatua gani wakandarasi wanojenga Barabara chini ya kiwango

“Serikali inapotoa nafasi ya ujenzi wa barabara hizi kwa wakandarasi inatarajia wakandarasi waweze kuzingatia mkataba wanapokuwa wanatekeleza ujenzi wa barabara hizi za wilaya na serikali inakuwa makini kusimamia viwango” amesema Mhe.Katimba

Katika swali la msingi la Mhe. Kamguna ameuliza lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha Lami

Akijibu Swali hilo Mhe. Katimba amesema “Serikali inakusudia kujenga kwa tabaka la lami barabara za makao makuu ya wilaya zote hapa nchini ikiwemo wilaya ya Malinyi na katika mwaka 2024/25”


“Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mnadani-Bomani inayoelekea Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa tabaka la lami (kilomita 0.85) kwa thamani ya shilingi 759,000,000.00 Mpaka sasa ujenzi bado unaendelea na umefikia 30%”. Mhe. Zainab Katimba

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora