logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA.

OR-TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali itaendelea kutenga na kupeleka fedha kwenye halmashauri zote nchini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya  vituo vya afya ili viweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Mhe.Dkt. Duagange ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki aliyetaka kujua
 lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaa tiba lakini hakina majengo ya kutosha.”

“Mheshimiwa Spika, Kituo cha afya Mwasayi kilianza kutoa huduma katika ngazi ya zahanati mwaka 1962 na kupandishwa hadhi mwaka 1977 na kuanza kutoa huduma ngazi ya kituo cha afya.
Aidha, majengo ya kituo hiki ni machache na chakavu.”

Amesema, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Mwasayi.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora