logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

SERIKALI KUENDELEA KUKARABATI VITUO VYOTE KONGWE, VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesema itaendelea kukarabati hospitali zote Kongwe kupitia mpango mkakati wa ukarabati, na upanuzi wa hospitali kongwe za halmashauri ,vituo vya afya Pamoja na Zahanati ili kuboresha miundombinu ya huduma za afya kote nchini.

Hayo yamesemwa leo Mei 07, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange  wakati akijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa , aliyetaka kujua ni lini serikali itaipa kipaumbele cha ukarabati wa miundombinu zahanati ya Rononi iliyoko Uru Kasikizini Mkoani humo.

Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema tayari serikali imeweka mpango mkakati wa ukarabati na upanuzi wa vituo vyote kongwe vya kutolea huduma za afya, ambapo tayari ukarabati na upanuzi umeanza katika ngazi ya hospitali kongwe za halmashauri, na baada ya hospitali za halmashauri, vitafutata vituo vya afya na zahanati zote kongwe ambazo zinahitaji ukarabati.

Hata hivyo Naibu waizri Dkt. Dugange ameelekeza wakurugenzi katika halmashauri zenye vituo vya kutolea huduma za afya vinavyokabiliwa na uhaba wa vifaa Pamoja na changamoto ndogondogo kama vile samani kutumia fedha za mapato ya ndani kumaliza changamoto hizo haraka iwezekanavyo.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora