logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

RHMT NA CHMT SIKILIZENI KERO NA MAONI KUTOKA KWA WANANCHI – DKT. MFAUME.

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume  amezielekeza timu za usimamizi wa afya ngazi ya Mkoa (RHMT) na ngazi ya Halmashauri (CHMT) kusikiliza kero na maoni kutoka kwa Wananchi pindi wanapotembelea kwenye vituo vya kutolea huduma za  afya kwaajili ya ziara za kikazi na ukaguzi.

Dkt. Mfaume amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kukagua  upatikanaji wa huduma za afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Katika Manispaa hiyo.

“Mara nyingi RHMT na CHMT tumekuwa tukifanya ziara za ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya bila kusikiliza mrejesho wowote kutoka kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa ziara hizo” amesema Dkt. Mfaume.

Amesema tusipopita na kusikiliza kero au maoni ya wananchi namna wanavyopokea huduma, uwekezaji wote ambao serikali umefanya katika ujenzi wa vituo vya afya, hospital na zahanati utakuwa hauna maana hivyo ni muhimu sana kuwasikiliza wananchi.

Aidha, Dkt. Mfaume amevielekeza vituo vya kutolea huduma za afya kwa kushirikiana na CHMT kutumia vizuri vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) katika kutangaza huduma zinazotolewa na vituo hivyo.

“Kuna huduma nyingi kubwa na muhimu sana ambazo hivi sasa Nchini zinatolewa hadi ngazi ya vituo vya afya lakini wananchi wetu hawana taarifa hivyo ni muhimu vituo na halmashauri kutumia wataalamu wetu katika vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) kutangaza huduma hizo kwa Wananchi” amesisitiza.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora