logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

OR – TAMISEMI yasisitiza ubunifu katika kuwekeza Miradi ya Maendeleo - Kimoleta

Ofisi ya Rais – TAMISEMI imewataka Makatibu Tawala wasaidizi sehemu za mipango, uratibu, uchumi na uzalishaji, wakuu wa idara za mipango na uratibu na waweka hazina wa halmashauri kubuni miradi ya maendeleo kwa kuzingatia mtaji wa rasilimali walizonazo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa tarehe 6 Juni, 2025 mkoani Dodoma  na Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Bi. Beatrice Kimoleta kwa niaba ya Katibu Mkuu OR – TAMISEMI, wakati akihitimisha mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo yaliyotolewa kwa muda wa siku nne kwa maafisa  hao yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi kabla ya kuanza kutekelezwa kwa bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026.

Bi. Kimoleta amesema imani ya Serikali baada ya mafunzo hayo ni washiriki kuwa wabunifu, kila mkoa na halmashauri hatua itakayopimwa kwa kuangalia namna maandiko ya uanzishwaji wa miradi ya vyanzo vipya vya mapato yalivyozingatia ubunifu na mtaji wa rasilimali walizonazo katika maeneo husika.

“Hatutegemei tena kuona kila halmashauri inawasilisha andiko la kujenga vituo vya mabasi (stendi)  yaani halmashauri zaidi ya 80 nyote mna wazo moja, tunachokiamini kuanzia sasa ni kuona maandiko yenye mawazo tofauti tofauti hasa yaliyozingatia kuwa eneo hili tuna rasilimali hii tukifanya mradi fulani utakuwa na tija kwa maendeleo ya jamii yetu, alisema Kimoleta.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora