logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI.42.4 KIGOMA,WADAU WAHIMIZWA KUUNGA MKONO SERIKALI

OR-  TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba  amepokea Vifaa vyenye thamani ya shilingi Mil.42.4 kwa ajili ya huduma za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha kwa Jamii.

Akipokea vifaa hivyo Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na miundombinu hiivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwemo Afya na Elimu” amesema

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu meneja wa NMB kanda ya Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, Viti  vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia  ambavyo vyote vimetolewa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda hamsini (50) kwa Wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Hata hivyo, vifaa vya Afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha Afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora