logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

Na OR – TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atupele Mwambene akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru kama Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, amefungua na kuendesha kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Green and Smart Cities Programme ambacho awali kilipokea taarifa ya utekelezaji wa kazi zinazoendelea na zitatolewa maamuzi katika kikao cha mwisho kinachotarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai, 2025.

Kwa upande wa Wadau wa Maendeleo Mwenyekiti mwenza Bw. Marc Stalmans Mkuu wa ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki ameshiriki kikao hicho na kufurahia mipango na makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Serikali ya Tanzania.

Aidha, kikao hicho kimepitisha masuala ya utekelezaji wa Mradi wa Green and Smart Cities kwa kuidhinisha Serikali ya Denmark kujiunga na Mradi huo ambapo Shilingi Bilioni 56 zinatarajiwa kupokelewa Serikalini, kuidhinisha matumizi ya fedha za mkopo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Shilingi Bilioni 189 na kuielekeza timu ya utekelezaji iweze kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi.

Kikao hiki cha Kamati Tendaji kimewahusisha Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanga na Mwanza, Watendaji kutoka Ofisi za Serikali zilizohudhuria, Wawakilishi kutoka Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar, mashirikia na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura