logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

Na John Mapepele

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya  nchini kuwaongeza wananchi katika maeneo yao kufanya "jogging" na mazoezi ili kuimarisha afya.

Mhe. Mchengerwa ametoa  maelekezo hayo leo Juni 14, 2025 mara baada ya kuongoza na kuhitimisha  mbio za pole pole (jogging) za kilomita 10 zilizoratibiwa na Wizara yake katika eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.

"Hamasa hii ya kufanya mazoezi iliasisiwa na viongozi wetu wakuu kuanzia enzi za Baba wa taifa letu Mwalimu Nyerere hadi Rais wetu wa sasa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa nyemelezi hivyo na sisi tuna wajibu wa kuendelea kuwahamasisha watumishi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye " amefafanua  Waziri Mchengerwa

Aidha, amewataka  watumishi wa TAMISEMI kujenga utamaduni wa  kufanya mazoezi wao pamoja na familia zao ili jamii yote iweze kuimarisha afya.

Amesema  utamaduni wa kufanya mazoezi ukijengeka siyo tu kwamba utasaidia kuimarisha afya bali utasaidia kupunguza gharama za kutibu magonjwa ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na tabia bwete.

Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kuwa na tabia za kupima afya zao badala ya kungojea hadi wanapoumwa.

Mbio hizo za pole zilizohudhuriwa na mamia ya watumishi wa TAMISEMI ziliishia katika jengo  la Ofisi ya TAMISEMI ambako kulikuwa na zoezi la upimaji wa afya kwa hiari.

Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Elimu zinaratibu Mashindano ya Michezo kwa Shule za Msingi ( UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) ambapo amefafanua kuwa mashindano hayo  yanasaidia kuibua vipaji vya wachezaji.

Amesema Serikali imeendelea   kuboresha  mashindano hayo ili kuwajengea utamaduni wa wanafunzi kufanya mazoezi  na kupenda michezo katika umri mdogo.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora