logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Mhe.  Mchengerwa atoa Tuzo ya Samia Kalamu Awards kwa Dodoma FM

Na John Mapepele

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI,  Mhe.  Mohamed Mchengerwa ameshiriki hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards 2025 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Akiwa katika tukio hilo, Mhe. Mchengerwa ametoa tuzo   kwa mtangazaji      Leila Sanga wa Dodoma Fm Radio kituo  ambacho kimeshinda tuzo ya kipengele cha redio za jamii.

Dodoma Fm Radio ni kituo kilichopo Dodoma,  kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na lengo la kuchangia maendeleo  ya mkoa wa Dodoma  katika nyanja mbalimbali.

Makala iliyoshinda katika tuzo hizi  inaitwa "Nani anaathirika na mabadiliko ya tabia nchi" ambapo iliangazia matumizi ya nishati safi yanavyoweza kuwapunguzia wanawake adha ya kufuata kuni umbali mrefu kitendo kinachowafanya kukutana na ukatili wa kijinsia ,pia matumizi ya nishati safi ya kupikia yanavyoweza kuokoa muda kwa mwanamke kufanya shughuli za kiuchumi.

"Tulifanya hivi kwa sababu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia 
Pia kuhamasisha jamii kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi 
Kuokoa wanawake na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa jamii ya Dodoma ambapo wanawake wengi wanalazimika kufuata kuni umbali mrefu". Amefafanua Sanga

Mgeni rasmi katika  tukio hilo amekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo alisistiza Waandishi wa Habari kuwa wazalendo kwa nchi yao wakati wanafanya kazi zao.

Aidha, amewataka kuelezea mafanikio na mageuzi yanayofanywa na Serikali.

Amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kazi nzuri vinayofanya kwa kutangaza miradi mbalimbali ya Serikali.

"Ndugu zangu hatusemi kuwa msiikosoe Serikali bali tunasema  tuwe wazalendo kwa nchi yetu kwa kuwa hatuna Tanzania nyingine" amesisitiza Mhe. Rais

Tuzo hizo ziliandaliwa na Chama  Cha Wanahabari Wanawake Tanzania na Mamlaka ya Mawasilino Tanzania ambapo tuzo  katika sekta mbalimbali zilitolewa.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora