logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

Mhe. mchengerwa atoa maagizo mahususi kwa marc na maded

OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amewaelekeza Wakuu wote wa mikoa kuwasimiamia Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia vipaumbele vya mwaka 2025/26 kikamilifu.

Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo Aprili 16, 2025 wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2025/26.

Amesema   vipaombele vya kuzingatia ni kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafikia malengo na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya afya ya msingi, elimu ya msingi na sekondari kulingana na mipango iliyowekwa.

Mhe. Mchengerwa amewaataka  kuzingatia kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidigitali ikiwemo uwekaji na matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma za afya na elimu.

Vilevile amewaagiza  kuhakikisha mapato katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa yanakusanywa kupitia mifumo ya TEHAMA ya Serikali pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mifumo hiyo ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

Aidha,  Mhe. Mchengerwa amesema Mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha inatekeleza Mikakati ya Uchumi wa Buluu, nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira.

Ameiagiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea  kuimarisha mifumo stahimilivu na endelevu ya utoaji wa huduma bora za afya, ustawi wa jamii na lishe ili kuboresha huduma ambayo ni nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote

Pia,  amewataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi kuhakikisha watoto walio chini ya miaka mitano wanajiunga kwenye vituo vya jamii vya kulelea watoto wadogo mchana.

“Kila halmashauri itapimwa utekelezaji wa vipaumbele hivi kwa kuzingatia miradi iliyotengewa bajeti kwa Mwaka 2025/26.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora