logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Mei 20, 2025 ameshiriki  kwenye zoezi la  kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Ikwiriri - Rufiji.

Mara baada ya kuboresha taarifa zake, Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi kote nchini kutumia muda wa siku mbili zilizobaki  kuboresha taarifa zao.

" Naomba kutoa wito kwa wananchi kwenda kuboresha taarifa zao katika kipindi hiki kifupi cha siku mbili ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa maendeleo ya taifa letu" amesisitiza Mhe waziri

Aidha, amefafanua kuwa zoezi la kuboresha taarifa ni la muhimu kwa kuwa taarifa hizo zinaweza pia kutumika na Serikali ili kuleta maendeleo.

Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kutumia vizuri hali yao ya kupiga kura wakati utakapofika.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora