logo

TAMISEMI

Students

YU
Yusuph Kajabukamakajabukama@gmail.com

MANYARA BINGWA RIADHA WASICHANA NA WAVULANA MITA 1,500

OR-TAMISEMI

Wanariadha wanaoshiriki Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi kutoka Mkoa wa Manyara, wameibuka kidedea katika mbio za mita 1,500 kwa upande wa Wasichana na Wavulana.

Mariam Gadiye, ameipa Manyara ubingwa kwa upande wa Wasichana, baada ya kutumia muda wa dakika 5:55:74 katika fainali   iliyofanyika juni 15,2025 kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Kleruu  Iringa.

Manyara pia imewika katika mbio hizo za mita 1,500 Wavulana,  baada ya Joshua Kidaghadawa kuibuka mshindi kwa kukimbia dakika 4:20:64 akifuatiwa na Apolinary D Apolinary pia wa Manyara aliyetumia dakika 4:26:68.

Nafasi ya tatu wavulana ilienda kwa Oreshiki Ndakaya kutoka Mkoa wa Arusha, aliyetumia dakika 4:26:92 na kuhitimisha Fainali hiyo ya UMITASHUMTA 2025 Riadha mita 1,500.

Aidha mkoa wa Kagera umefanikiwa kuibuka na ubingwa wa riadha upande wa Mita 400,kufuatia ushindi wa Dominko Mikoduni aliyetumia muda wa sekunde 54:90 akifuatiwa na Maseto Elenjori wa Arusha sekunde 55:27.  

Wasichana mita 400 Ubingwa umeenda Mkoa wa Shinyanga,  baada ya Rehema Nyalu kukimbia kwa muda wa dakika 01:03:41 akifuatiwa na Catarina Charles wa Mwanza dakika 01:04:38.

Katika fainali ya Mita 100,  Janeth Mhebule kutoka mkoa wa Mwanza alimaliza katika nafasi ya kwanza akitumia muda wa sekunde 13:13, na upande wa Wavula Mkoa Mara uliibuka na ushindi kupitia kwa Anold Mkomangiwa ubingwa aliyetumia sekunde 11:65

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura