logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

MAHUSIANO MAZURI KATI YA SERIKALI NA TAASISI ZA DINI NI CHACHU KATIKA  HUDUMA  BORA ZA AFYA.

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii , Ofisi ya  Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amesema mahusiano mazuri kati ya Serikali na taasisi za dini yamekuwa chachu katika kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Dkt. Mfaume ameyasema hayo hivi karibuni  mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Cardinal Rugabwa inayomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki la  Dar es Salaam katika ziara yake inayoendelea mkoani huku yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.

“Hapa tunaona mitambo kikubwa ya kutolea huduma za afya, Serikali imeiweka mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini zote ikiwa ni pamoja na uwekezaji kwenye Sekta ya afya” amesema Dkt.Mfaume

Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka timu za usimamizi wa afya (CHMT) katika Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi hizo kwa kuwa zinatekeleza majukumu hayo kwa niaba ya Serikali.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Sr.Dkt. Sarah Deogratius amesema ziara ya Mkurugenzi katika Hospitali hiyo imewatia moyo wa  kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora