logo

TAMISEMI

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz

LAAC yataka dosari zilizobainishwa na CAG Halmashauri ya Wilaya Kilolo zitatuliwe

Na OR-TAMISEMI, Kilolo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),  imeielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuhakikisha inaziondoa dosari zote zilizobainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Lugalo, mkoani Iringa.

Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa kamati, Halima Mdee baada ya kamati kutembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo.

"Dosari zote zilizobainishwa na CAG katika utekelezaji wa mradi huu zinaondolewa na kuhakikisha miundombinu muhimu inakamilika," amesema Mhe. Mdee.

Kamati pia imeelekeza Afisa Masuuli wa Halmashauri kuandaa taarifa yenye maelezo ya kina na mchanganuo wa matumizi ya fedha zote za mradi huo na kuiwasilisha kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.

Aidha, kamati imeitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kufanya tathmini ya kina na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo, huku ikichukua hatua za haraka iwapo kutabainika ukiukwaji wa sheria na taratibu.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Habari na Matukio

Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.

Cookie

We use cookies to enhance your browsing experience, provide personalized content, and analyze our traffic. By clicking "Accept All Cookies", you agree to the storing of cookies on your device to improve site navigation, analyze site usage, and assist in our marketing efforts. To learn more about how we use cookies and to manage your preferences, please visit our Cookie Policy.
National Election Commission Logo

Uchaguzi 2025

Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora