
Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari
Also known as: SEQUIP
About this Project
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI wanatekeleza Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP). Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia yanaboreshwa katika shule za Sekondari. Mradi unatarajiwa kutekelezwa katika eneo la Elimu ya Sekondari Kidato cha Kwanza hadi cha Sita kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2020/2021 hadi 2024/2025. Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wa fedha za Kimarekani Dola milioni 500 sawa na fedha za Kitanzania Shilingi Trilioni 1.2

