• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Waziri Jafo amtaka Ras Pwani kuanza na Miradi ambayo haijakamilika

Imewekwa tar.: May 22nd, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amemtaka Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Pwani Dkt. Delphine Magere kuanza utendaji kazi wake kwa kufanyia kazi  miradi ya mabweni, mabwalo na vituo vya afya ambavyo havijakamilika kwa wakati kwani ni miradi iliyotumia pesa nyingi na muda mrefu katika Mkoa huo.

Mhe. Jafo ametoa kauli hiyo leo wakati Dkt. Magere alipokuja kuripoti OR-TAMISEMI Mtumba Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli na kukabidhiwa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na Kitabu cha Bajeti 2020/21, Mafanikio ya Miaka Minne ya OR-TAMISEMI,Sheria ya Tawala za Mikoa pamoja na nyaraka zingine mbalimbali.

Akizungumza Mhe. Jafo amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kufanya ujenzi na maboresho katika sekta ya Elimu na Afya Mkoani pwani na baadhi ya Halmashauri zingine hazifanyi vizuri katika usimamizi wa miradi hiyo.

“Dkt.Magere hakikisha unasimamia mabweni, mabwalo, vituo vya afya na Hospital za Wilaya ambazo zinaendelea kujengwa na kukarabatiwa, kazi hiyo ifanyika kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa, hakikisha force account inatumika katika miradi hiyo na inakamilika kwa wakati”, ameelekeza Mhe.Jafo.

Aidha Mhe. Jafo amemtaka Dkt. Magere akasimamie ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa kuwa vimeshafika kwenye Ofisi za Mamalaka ya Mapato ya Mikoa na vinatakiwa kuwafikia walengwa haraka iwezekanavyo.

Halkadhalika alisisitiza Dkt. Magere kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri zote na kuhakikisha fedha hizo  zinatumika kwa kuzingatia taratibu sahihi.


“Ukusanyaji wa mapato uzingatia matumizi ya mashine za kieletroniki ili kusaidia kupunguza upotevu wa fedha za Serikali na kuongeza mapato ya halmashauri ili ziweze kujiendesha na kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea Ruzuku toka Serikali kuu na kwa wafadhili” alisema Jafo.

Mhe. Jafo alimalizia kwa kumsisitiza Dkt. Magere  kusimamia nidhamu ya watumishi, matumizi mazuri ya rasilima za taifa na uwajibikaji ili kuleta utendaji mzuri katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Pwani.

Naye Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga amempongeza Dkt. Magere kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kumtaka kuchapa kazi ili kuleta matokeo chanya kwa Mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Katibu Tawala  Mkoa wa Pwani Dkt. Delphine Magere amesema kuwa anamshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa nafasi hii na amekwishakuanza  kazi hata kabla ya kuapishwa kwa kutembelea Wilaya 6 na Halmashauri 7 za Mkoa wa Pwani.

“Nazidi kuwaomba wananchi na watumishi wote wa Mkoa wa Pwani tushirikiane katika kuchapa kazi ili kuleta maendeleo katika mkoa wa Pwani na Taifa kwa Ujumla” alisema Dkt. Magere.

Na. Majid Abdulkarim- TAMISEMI

 



Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MSIKWAMISHE MIRADI YA SEQUIP - Silinde

    June 29, 2022
  • Wataalam wa Maabara na Wafamasia waaswa kusimamia vifaa tiba

    June 29, 2022
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA, ELIMU NA AFYA - MSOMERA HANDENI

    June 22, 2022
  • FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 21, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.