Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

WANAFUNZI 188,787 WACHAGULIWA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2024

Imewekwa tar.: May 31st, 2024

WANAFUNZI 188,787 waliokidhi vigezo wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 812 wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati nchini kwa mwaka 2024. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

Haya yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa wakati wa kuzungumzia uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi. Amesema Uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa.

 “Hivyo, Wanafunzi wote 188,787, waliokidhi vigezo wakiwemo wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 812 wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati katika fani mbalimbali.” Mchengerwa alisema wanafunzi 131,986 wakiwemo wasichana 66,432 na wavulana 65,554 wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano 622 zikiwemo shule mpya 82 zinazoanza mwaka huu. 

Alisema kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 1,462 wakiwemo wasichana 669 na wavulana 793 wamepangwa katika shule za sekondari 8 zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls. Pia wanafunzi 6,576 wakiwemo wasichana 3,449 na wavulana 3,127 wamepangwa katika Shule za Sekondari za Kutwa za Kidato cha Tano, Alisema pia wanafunzi 123,948 wakiwemo wasichana 62,636 na wavulana 61,312 wamepangiwa katika shule za Sekondari za Bweni za Kitaifa za Kidato cha Tano. 

Aidha, Mchengerwa alisema wanafunzi 56,801 wakiwemo wasichana 17,332 na wavulana 39,469 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi na fani mbalimbali za Stashahada katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET). 

Alisema kati ya hao wanafunzi 2,107 wakiwemo wasichana 804 na wavulana 1,303 wamechaguliwa kujiunga katika Vyuo vinne vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji (WDMI). 

Pia wanafunzi 2,019 wakiwemo wasichana 1,011 na wavulana 1,008 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada. Alisema pia wanafunzi 52,675 wakiwemo wasichana 15,717 na wavulana 37,158 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali zikiwemo za Kilimo, Ufugaji, Utawala, Biashara na zinginezo za Stashahada katika Vyuo Elimu ya Ufundi mbalimbali nchini. 

Aidha, Mchengerwa alisema Serikali imehakikisha wanafunzi wote wenye sifa wamepata nafasi kwenye shule na vyuo vya elimu ya ufundi. "Hili ni lengo la Serikali kuendelea kutoa huduma kwa Watanzania wote na haswa wakati huu tunaotoa elimu bila ada.” 

“Nipende kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha miundombinu ya Elimu inapatikana ambayo imewezesha wanafunzi wote waliokuwa na sifa kuchaguliwa kidato cha tano na vyuo.” 

Aidha, Mchengerwa alisema muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza Julai Mosi mwaka huu na kuwataka wanafunzi waliopangwa kujiunga na Kidato cha Tano kaunza kuripoti shuleni kuanzia Juni 30 mwaka huu. 

“Siku ya mwisho ya kuripoti shule walizopangiwa itakuwa tarehe 14 Julai mwaka 2024.” Mchengerwa alisema kwa wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi watapokea maelekezo ya namna ya kujiunga kutoka katika vyuo walivyopangwa.

 “Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule, hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi.” 

“Wazazi na walezi wote tuendelee na moyo huu wa kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto ikiwemo kuwalea katika malezi na maadili mema ili wawe raia wema na wanaotegemewa na Taifa letu.”

 Mchengerwa pia amewataka wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kuendelea kufanya bidii katika kujifunza ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita na Vyuo vya Elimu ya Ufundi. 

Mchengerwa pia amewataka wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa azma ya Serikali ya kuwa na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano katika kila Tarafa inatekelezwa. 

“Hii itawezesha wanafunzi wote wanaofaulu Mtihani wa Kidato cha Nne kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano na Sita.” “Upanuzi na ujenzi wa Shule Mpya za Kidato cha Tano na Sita uendelee kufanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza tahasusi za masomo ya Sayansi. 

Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi na walezi na wanafunzi gharama za usafiri kwenda shule za mbali.” 

Watahiniwa 572,359 walifanya mtihani wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2023, watahiniwa wa shule walikuwa 543,332 na wa Kujitegemea ni 29,027. 

Aidha, ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja, unaonesha kuwa watahiniwa 197,426 sawa na asilimia 37.42 walipata ufaulu wa Daraja la I – III, hali inayoonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2023 umeongezeka kwa asilimia 0.47 ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I – III wa watahiniwa 192,348 asilimia 36.95 wa mwaka 2022.


Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.