• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

WAKUU WA IDARA SIMAMIENI MIRADI-MAJALIWA

Imewekwa tar.: February 15th, 2023

OR - TAMISEMI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara katika Halmashauri zote nchini wasimamie kikamilifu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao na wahakikishe inakamilika kwa wakati ili itoe huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

“Huduma za jamii ndizo zinazogusa maisha ya kila siku ya wananachi kama elimu, maji, nishati, afya na kilimo, hivyo Halmashauri zetu lazima ziongeze nguvu katika maeneo hayo. Wakuu wa Idara tumieni muda mwingi kwenda kwenye maeneo ambayo miradi inatekelezwa badala ya kukaa ofisini tu.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2023) wakati akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi Mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kujenga baadhi ya miradi kwa kutumia makusanyo ya ndani ukiwemo ujenzi wa madarasa 10 katika shule ya msingi haisoja kwa gharama ya shilingi milioni 800, amewataka viongozi wa Halmashauri zingine nchini kuiga mfano huo.

“Viongozi wa Halmashauri muwe wabunifu na mtumie fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yenu ili ziwasaidie katika kuongeza mapato. “Shirikisheni na sekta binafsi hawa watawasaidia kuleta maendeleo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha mwelekeo kwenye hili. Tambueni mchango wao, lengo la Serikali ni kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewaelekeza viongozi wa Wilaya, Halmashari na wawakilishi wa wananchi waimarishe ushirikiano baina yao na watumishi wengine katika maeneo yao ili kuhakikisha azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo inafikiwa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) waongeze wigo wa kufanya tafiti za maeneo ambayo maji yatapatikana sambamba na kuongeza ulinzi kwenye vyanzo vya maji ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa maji inatatuliwa. “Pia viongozi wa Halmashauri tushirikiane kulinda vyanzo hivyo.”

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza Wakaguzi wa Elimu nchini wapite kwenye shule zote wakakague vitabu vinavyotumika katika shule hizo kama vinaendana na maadili na tamaduni za Kitanzania. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameelekeza tusimamie maadili yetu, mila zetu, desturi zetu na utamaduni wetu wa Kitanzania.”

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 190 kupelekwa mkoani humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maedndeleo ikiwemo ya afya sh. bilioni 47, maji sh. bilioni 30. 7, elimu sh. bilioni 32.9, nishati sh. bilioni 53.4 na barabara sh. bilioni 27.5


Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.