Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

Imewekwa tar.: January 21st, 2021


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ameiagiza Mikoa ambayo Halmashauri zake zimekusanya mapato chini ya asilimia 50 kufanya tathmini na kuweka mikakati madhubuti katika ukusanyaji wa mapato katika vipindi vilivyosalia.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/21 kwa kujumuisha taarifa ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani vya Halmashauri kuanzia Julai hadi Desemba, 2020.

Waziri Jafo amesema wakurugenzi wa Halmshauri  zote ambazo hazijafikia asilimia 50 ya makisio kwa kipindi hiki cha nusu mwaka wanatakiwa kujitathmini na kuweka mikakati mizuri ya kufikia malengo  katika ukusanyaji wa mapato.

Ameendelea kusisitiza kuwa kila Halmashauri kuendelea kutumia kwa usahihi mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na mifumo ya uhasibu ili kutoa taarifa kwa kufuata matakwa ya kisheria na kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta za Umma (IPSAS).

Akizungumzia ukusanyaji wa Mapato hayo Waziri Jafo ameeleza kwa mwaka  wa fedha 2020/21 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 814.96 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Desemba, 2020 Halmashauri  zimeweza kukusanya  jumla ya shilingi bilioni 381.27 sawa na  asilimia 47.

Amefafanua kuwa taarifa za mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri katika kipindi cha Julai - Desemba, 2020 imeonesha uwepo wa ongezeko la mapato yaliyokusanywa kuwa ni shilingi bilioni 24.5 ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho cha Julai - Desemba, 2019 sawa na ongezeko la asilimia 7.

Waziri Jafo ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 88 ya makisio yake ya mwaka wakati Halmashauri za Wilaya za Kishapu na Longido zikiwa za  mwisho kwa kukusanya chini ya asilimia 20 ya makisio yake ya mwaka.

Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi bilioni 30.67 na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 324.89.

Hata hivyo katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo Waziri Jafo amebainisha kuwa Mkoa wa Katavi umefanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo umekusanya kwa wastani wa asilimia 62 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo wakati Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Simiyu ambao umekusanya wastani wa asilimia 36 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameweka wazi Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa Kuzingatia Wingi wa Mapato kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kigezo cha wingi wa mapato   ambapo imekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 89.13 huku Mkoa wa mwisho katika wingi wa mapato ni Mkoa wa Rukwa ambao umekusanya Shilingi Bilioni 4.07.

Vile vile Ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa Kuzingatia aina ya Halmashauri kwa Kigezo cha asilimia ya makusanyo ukilinganisha na makisio  ya mwaka Waziri Jafo amesema kwa upande wa Majiji Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 50 ya makisio yake ya mwaka na Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya kwa asilimia 39 ya makisio yake ya mwaka.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa ambayo imekusanya asilimia 69 ya makisio yake na Katika kundi hilo Halmashauri ya Manispaa ya Singida imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya kwa asilimia 29 ya makisio yake ya mwaka.  

“Kwa kundi la Halmashauri za Miji , Halmashauri ya Mji wa Kahama imeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 67 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Halmashauri ya Mji wa Bariadi imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 23 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21” amesema Waziri Jafo

Aidha, kwa upande wa Halmashauri za Wilaya amesema Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya asilimia 88 ya makisio ya mapato ya ndani huku Halmashauri za Wilaya za Kishapu na Longido zimekuwa za mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya chini ya asilimia 20 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa Fedha 2020/21.

“Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kundi la Halmashauri za Majiji kwa kigezo cha wingi wa mapato kwa kukusanya Shilingi bilioni 18.53 na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi bilioni 5.66.” ameeleza Waziri Jafo

Kwa kuongezea Waziri Jafo amesema kwa upande wa Halmashauri za Manispaa,Manispaa ya Ilala imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 30.70 na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 834.53,

Huku katika kundi la Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 4.78. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 324.89


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.