Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waganga Wakuu wa Wilaya watakiwa kusimamia uwekaji kumbukumbu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya

Imewekwa tar.: June 20th, 2021

Na Mwandishi wetu, Morogoro

Serikali imewataka Waganga wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha kuwa wanawasimamia watendaji wa vituo vya kutolea huduma za afya kuweka kumbukumbu za dawa, vifaa tiba, vitendanishi vinavyonunuliwa pamoja na mapato yatokanayo na huduma hizo.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Mvomero.

Amesema kuanzia sasa hatarajii kuona kituo cha kutolea huduma ya afya nchini kutokuwa na kumbukumbu ya dawa, vitendanishi na vifaa tiba pamoja na kutokuwa na taarifa za mapato ya kituo husika cha kutolea huduma za afya.

Agizo la Naibu Waziri linafuatia ziara yake katika hospitali ya Wilaya ya Mvomero na kukuta Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo kushindwa kueleza kumbukumbu za dawa, vifaa tiba, vitendanishi pamoja na mapato ya hospitali hiyo licha ya hospitali hiyo kuwa na dawa zote muhimu zinazohitajika.

Amesema serikali haipo tayari kuona mali inazonunua zinapokelewa na zinatumika bila kuwa na kumbukumbu zinazotakiwa.

“Tukifika katika kituo tukute mtiririko wote wa kumbukumbu zote umeainishwa, wahusika wamesaini, na hizo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinaonekana na kama vimetumika tunajua nani ametumia,” amesema Dkt Dugange.

Amesema serikali inapotaka kununua dawa asihusike mtu mmoja peke yake maamuzi ya dawa zipi zinunuliwe, za shilingi ngapi, zinanunuliwa wapi, yafanywe na kamati ya matibabu ya kituo ambayo ina wajumbe kadhaa, ambao watasaini na kukubaliana kuwa inakwenda kununua dawa hizi.

“Dawa zikishanunuliwa ni lazima zipokelewe na wajumbe wale, wazihesabu, wajiridhishe, waweke na saini zao kwamba tumepokea dawa hizo na ziingizwe kwenye leja na zinapotoka bohari kuu ziende kwenye bohari ndogo na kwenda kwa mgonjwa ili kila sehemu nani alizitoa hapa na kuzipeleka dispensing, akapeleka kwa wagonjwa nani ni mgonjwa gani alipata zile dawa,” amesisitiza Naibu Waziri na kuongeza:

“Bado sijaridhishwa na ufanisi wa makusanyo ya huduma za uchangiaji katika hospitali yenu Mvomero, Mganga mfawidhi hujui kwa siku anakusanya shilingi ngapi, katika seksheni ipi tunachotaka kila sehemu ijipime, maabara ijipime wao wanachangia kiasi gani kwa siku, kwa mwezi na kwa mwaka, dawa wajipime, wodi ya watoto wajipime, kwa sababu hivyo vyote ndiyo vyanzo vya huduma, lakini pia ndiyo vyanzo vya mapato,” amesema.

Naibu Waziri aliwataka watendaji wa vituo vya kutolea huduma za afya nchini kuondokana na fikra ya utegemezi  na kwamba sasa sekta ya afya iwe na uwezo wa kusimama kwa miguu yake huku ikisaidiwa fedha kutoka serikali kuu,” amesema na kuongeza:

“Tusiwe wategemezi asilimia 99 wa fedha ya serikali kuu, ya MSD haiwezekani, kwa sababu sisi tunazalisha, tunatoa huduma, tunachangiwa huduma ya fedha lazima zionekane ni kiasi gani kwa siku, zimekwenda wapi, zinatumika wapi. Hili nimewapa siku 21, nataka nije nione taarifa kabisa ambayo inaeleza kila seksheni inachangia kiasi gani.”

Dkt Dugange pia amewaagiza watendaji hao kuweka benki kwa wakati fedha wanazokusanya kwa kuzingatia huduma ya kibenki ipo karibu na hospitali.

” Benki ipo hapa ndani ya mita kadhaa, lakini ninyi kwa mwezi kwa mfano mei mmeingiza mara 6 tu katika siku 31, siku 25 fedha zilizokusanywa zinakwenda wapi, namuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mganga Mfawadhi, nataka nipate taarifa ya mapato ya mwezi wa tano wote yaliyokusanywa hapa ambayo yatakuwa na ushahidi kwenye mfumo na nikiwa na mashaka nitarudi, na nikiona mmetoa taarifa isiyo sahihi hali yenu haitakuwa nzuri,” amesisitiza Naibu Waziri.

Pia Naibu Waziri ameagiza apate taarifa ya mapato ya hospitali kwa mwaka mzima ili ijulikane hospitali inapata shilingi ngapi kwa wastani, Januari hadi mwezi wa sita wanapata shilingi ngapi kila mwezi.

Dkt Dugange amesema kuanzia sasa angependa kuona kila kituo cha kutolea huduma kinakuwa na utaratibu huo na amesema utakuwa endelevu. 

“Hakuna jambo tunahitaji kusisitiza kama kuhakikisha tunaziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali,” amesema.

Aidha Naibu Waziri amewaonya  baadhi ya watumishi wa serikali wasio waaminifu ambao wanatumia vibaya fedha za makusanyo katika vituo vya kutolea huduma na wanapelekea vituo hivyo kuwa na fedha kidogo kuacha tabia hiyo mara moja.

“Misamaha inasingiziwa sana pamoja tunajua tuna mzigo wa msamaha lakini kuna feki exemption nyingi,” amesema Dkt Dugange.

Amewataka Waganga Wakuu wa Wilaya nchini kuhakikisha wanaweka mifumo mizuri ya kuratibu nani anastahili kusamehewa na kweli amesamehewa.

Ameongeza kuwa wapo baadhi ya watumishi wachache ambao wanatumia fursa ya misamaha kudanganya, kujipatia mapato ya udanganyifu na wanaandika kwamba hii ni misamaha.

“Nielekeze na nitalifuatilia kwa karibu sana nataka tukiambiwa hii ni misamaha tuone ipo wazi kwamba ni misamaha na ni nani tukitaka kumtrace mnufaika wa msamaha tumpate,” ameagiza.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya alimuahidi Naibu Waziri kuwa maagizo yote aliyoyatoa yatatekelezwa na taarifa atazipata ndani ya siku 14 badala ya siku 21 alizotaka Naibu Waziri.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.