• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

VIONGOZI WA ELIMU MSIKAE OFISINI FUATILIENI UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI MASHULENI- DKT. DUGANGE

Imewekwa tar.: January 9th, 2023

OR - TAMISEMI - NJOMBE

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo  Dugange amewataka viongozi wa Elimu ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mikoa kutokaa ofisini bali wafuatilie ufundishaji na ujifunzaji shuleni kwa kushauriana na walimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata umahiri uliokusudiwa katika masomo yote.

Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo tarehe 9 Januari 2023 mkoani Njombe katika Mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa Elimu msingi na sekondari uliowakutanisha viongozi wa Elimu ngazi zote.

“Viongozi wa Elimu jielekezeni zaidi kufuatilia ufundishaji wa walimu darasani na kutatua kero za walimu kwenye maeneo yao ya kazi na mhakikishe mnaimarisha uwajibikaji wa watumishi wote katika ngazi zote ili kuongeza tija katika utendaji wa kazi” amesisitiza Dkt. Dugange

Amewataka Walimu kujiwekea malengo yao binafsi katika masomo wanayofundisha na kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayeshindwa kupata umahiri uliokusudiwa katika somo lake analofundisha.

Dkt. Dugange amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya  mambo makubwa na  anaendela kuwekeza katika elimu ambapo ameendelea kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 29.82 kila Mwezi kwa ajili ya Elimu bila ada.

Aidha, Dkt. Dugange ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Shilingi Bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya nchi nzima kwa ajili ya kupokea wanafunzi kidato cha kwanza mwaka 2023 ambao wameanza kupokelewa mashuleni leo.

Hadhalika, amesema Serikali inaendelea kuwekeza pesa nyingi katika Sekta ya elimu kupitia miradi mbalimbali kama mradi wa kuimarisha Elimu ya Sekondari  SEQUIP wa Shilingi Trilioni 1.2, mradi wa kuimarisha Elimu ya Msingi BOOST wa Shilingi Trilion 1.15.

Wakati huo huo, Dkt. Dugange ameeleza mafanikio ya Katika Sekta ya Elimu ambapo idadi ya Wanafunzi wa elimumsingi wameongezeka kutoka wanafunzi 11,877,565 mwaka 2016 hadi 15,609,931 mwaka 2022 pia idadi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita iliongezeka kwa asilimia 35.86 kutoka 131,362 mwaka 2016 hadi 178,473 mwaka 2022.

Pia, ameeleza ongezeko la ufaulu wa mitiani ambapo Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi umeongezeka kutoka asilimia 70.40 mwaka 2016 hadi asilimia 79.62 mwaka 2022,  Ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha nne umeongezeka kutoka asilimia 70.35 mwaka 2016 hadi asilimia 87.30 mwaka 2021 na  kidato cha Sita, ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.94 mwaka 2016 hadi asilimia 99.87 mwaka 2022.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTWA KAZINI September 13, 2023
  • Terms of Reference TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS PROJECT (TACTIC) September 01, 2023
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI,2023 September 22, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA MPYA 2023 AWAMU YA PILI August 30, 2023
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KWA SHULE MPYA ZA SEKONDARI,2023 August 25, 2023
  • KUSIMAMISHWA KAZI KWA MKURUGENZI WA BUHIGWE July 12, 2023
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATAALAM WA ELIMU

    September 18, 2023
  • DKT. SAMIA ASHANGAZWA NA HALMASHAURI KUSHINDWA KUJENGA JENGO LA X-RAY

    September 17, 2023
  • SHULE ZA MSINGI 1,000 KUJENGWA NCHI NZIMA

    September 17, 2023
  • TRILIONI 6.5 ZATEKELEZA MIRADI YA ELIMU, AFYA NA MIUNDOMBINU

    September 15, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.