Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Vikundi 182 Kigamboni vyapewa Mikopo ya Shilingi Milioni 616

Imewekwa tar.: March 15th, 2021

Na Ada Phestor, Kigamboni

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 616 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo kwa vikundi 182 vya wanawake, vijana na walemavu katika mwaka wa fedha 2019/20 .

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Erasto Kiwale amesema fedha hizo zilitolewa kwa vikundi 126 vya wanawake, 51 vijana na vikundi 5 vya walemavu.

Amesema mikopo hii imekuwa na tija kwa wakazi wa Kigamboni kwani imeweza kukuza mitaji ya wajasiriamali, na kuwatoa wajasiriamali kwenye mitaji midogo waliyokuwa nayo mfano mamalishe aliyekuwa na mtaji wa laki 3 kupitia mfuko huu umemuwezesha kuwa na mtaji wa milioni 3.

Ameongeza kupitia mikopo hii vijana wengi wameweza kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha miradi na kupata mikopo inayowasaidia kujiendeleza kiuchumi na kupunguza wimbi la vitendo vya uhalifu hali iliyopelekea kuwa na utulivu katika Mji wa kigamboni .

Miongoni mwa vikundi vilivyopata mikopo hiyo ni Kikundi cha Vijana wa Gonga gonga ambacho kinajihusisha na ufundi selemala wa kutengeneza Samani mbali mbali.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho Hashim Shelukindo amekiri kikundi chake kunufaika na Mkopo wa Manispaa hiyo ambapo waliweza kupokea kiasi cha Shilingi Milion 8 ili kuboresha shughuli zao na hiyo ni kwa sababu ya juhudi na jitihada zao katika urejeshaji.

“Tunaishukuru Manispaa, inajali sana kikundi chetu na ni sababu hatusumbui kwenye marejesho, mkopo umetuwezesha kuboresha biashara na ofisi kwa ujumla hivyo tunaomba wakati mwingine tukiomba mkopo tupate kiasi tuhachohitaji sababu hatusumbui kurejesha,”amesema Shelukindo

Kwa upande wake Katibu wa kikundi cha Kona Bar ambacho kinanufaika na mkopo wa pikipiki 3 zenye thamamni ya Milion 8, Sande Patric amesema kabla ya kupata mkopo huo walikuwa wanafanyia kazi pikipiki za watu binafsi ambazo zilikuwa zikiwabana kwenye muda wa utendaji kazi lakini pia kipato.

Ameongeza kuwa wao kama kundi wamelenga kuhakikisha kila mwanachama anapata pikipiki yake kwa mikopo hii ya serikali ambayo imewapa ari ya kufanya kazi kwa bidii ili warejeshe mikopo hiyo bila tatizo hatimaye wajumuishwe tena kwenye mikopo mingine.

Nacho Kikundi cha watu wenye ulemavu cha fighting against poverty group kimeishukuru serikali kwa kuwapa fursa watu wenye ulemavu na kuwaondolea hali ya utegemezi na kuombaomba kwa kujiunga na vikundi vya kiuchumi vinavyowawezesha kujitegemea na kuhudumia familia zao.

Mjumbe wa kikundi cha fighting against poverty group Khamis Wana amesema kuwa Manispaa iliwapatia mkopo wa  bajaji 5 wenye thamani ya Milioni 39.8 ambazo zimewapatia ajira ya kuingiza kipato na kuondokana na hali ya utegemezi.

“Tunaishukuru Serikali tunaomba iwasaidie hata na walemavu wengine ambao mitaji yao ni midogo kwaajili ya shughuli ndogo kama machinga ili nawao waweze kujikwamua kupata riziki zao wenyewe”amesema Khamis.

Naye katibu wa kikundi cha Tushikamane Habiba Mhina amesema kuwa wanashukuru kupata mkopo wa Manispaa kiasi cha Milioni 3 zilizowawezesha kununua mashine ya kuchomoleaa ambayo hapo awali hawakuwa nayo na kununua vyuma na vifaa vingine ili kukuza biashara yao ya utengenezaji wa samani kwa kutumia vyuma na uchomeleaji wa Vitanda,madirisha ,mageti n.k.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kigamboni Happy Luteganya amesema kwamba wataalamu wa maendeleo wapo kuanzia ngazi ya Kata ambapo elimu ya uandaaji wa vikundi namna ya miradi yenye tija inatolewa kwa wanavikundi kabla ya kupewa mikopo, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vyote vilivyokidhi sifa, namna ya kutunza kumbukumbu, usimamizi wa miradi na utafutaji wa masoko.

Afisa maendeleo ameendelea kwa kusema baada ya kupewa mikopo vikundi hivi vinakuwa kwenye usimamizi wa karibu ili kuona mikopo waliyopewa inaenda kutumika kwenye miradi waliyoomba na kuleta tija.

Mbali na changamoto ya urejeshaji wa mikopo kwa baadhi ya vikundi hususani vya vijana na watu wenye ulemavu Afisa Maendeleo ya Jamii bado anahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuunda vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo isiyo na riba ili kuepukana na mikopo mingine yenye riba kubwa zinazowafunga kwenye kutimiza malengo yao.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.