Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Timu ya Ufuatiliaji yakerwa na kususua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale Mkoani Simiyu

Imewekwa tar.: June 17th, 2019

Timu ya ufuatiliaji inayoshughulika na Mradi wa Huduma ya Afya ya  Uzazi na Mtoto kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI imekerwa na kusuasua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu .

Akiongea kwa niaba ya Timu hiyo Mratibu wa Mradi wa Afya  ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi.  Dinah Atinda amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya vitu vingi kutokamilika na jengo hilo kutotumika licha ya kutakiwa kuanza kutoa huduma za mama na mtoto katika jengo hilo.

Ameyataja maeneo ambayo hayajakamilika kuwa ni uwekaji wa milango,  ufungaji wa gata za kuvunia maji, uwekaji  wa madirisha ya alluminium,  uwekaji wa  mfumo wa umeme, uwekaji wa marumaru  upande wa vyooni , uchimbaji na ujenzi wa mashimo ya maji taka, uwekaji wa  masinki wakati fedha zote zilitolewa kwa ajili ya ujenzi  ambapo ujenzi huo ulikuwa unatakiwa kukamilika juni, 2018

“Ni jambo la kushangaza kuona Zahanati iliyotakiwa kuanza kutumika tangu 2018 mpaka leo haijaanza kufanya kazi japokuwa Serikali imeweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, suala hili halipendezi na linarudisha nyuma maendeleo kwa jamii” amesisitiza Bi. Atinda

Amesema kuwa timu imegundua kuwa kuna matumizi ya fedha yasiyofuata  miongozo yaliyofanywa wakati wa ujenzi wa miundombinu ya Zahanati hiyo ambapo taarifa zinaonyesha kuwa Fundi wa ujenzi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 5 kati ya shilingi milioni 6 alizotakiwa kulipwa wakati sehemu kubwa ya ujenzi huo haujakamilika.

Bi. Atinda ameiagiza Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa jengo hilo na kuanza kutumika ifikapo tarehe 30 juni, 2019 na kutumia fedha zilizopelekwa na TAMISEMI katika robo ya nne ya mwaka 2018/2019 kufanya usimamizi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya 38 vilivyofanyiwa maboresho chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA na kuhakikisha vituo vyote vinaanza kutoa huduma kwa jamii.

Bi. Atinda amesema kuwa tathimini ya matumizi ya fedha iliyofanywa na mkaguzi wa ndani wa Halmashaiuri ya Mji wa Bariadi ifanyiwe kazi na kutolewa taarifa  katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Aidha Timu ya Ufuatiliaji kutoka OR-TAMISEMI ilifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi na matumizi ya Zahanati na Vituo vya afya vilivyojengwa Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMCH-UNFPA.

Na, Angela Msimbira SIMIYU




Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.