Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TAMISEMI yaomba tril. 10.125

Imewekwa tar.: April 16th, 2024

OR-TAMISEMI

OFISI ya Rais - TAMISEMI, taasisi zilizo chini yake, mikoa 26 ikijumuisha halmashauri 184 zimeomba Bunge kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2024/25 yenye jumla ya  shilingi trilioni 10.125.

Kwa mwaka 2023/24, Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliidhinishiwa bajeti ya  trilioni 9.18, kati ya fedha hizo, trilioni 3.52 ni fedha za maendeleo na trilioni 5.65 ni za matumizi ya kawaida na hadi kufika Machi, 2024 ofisi imekusanya na kupokea trilioni 6.99 sawa na asilimia 76.18 ya fedha zilizoidhinishwa na kati ya hizi trilioni 4.47 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na trilioni 2.52 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikijumuisha trilioni 2.06 fedha za ndani na bilioni 456.39 fedha za nje.

Haya yamebainishwa leo  Aprili, 16, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na taasisi zake kwa mwaka 2024/25.

Amesema kati ya fedha zinazoombwa, zaidi ya trilioni 6.71 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati zaidi ya trilioni 3.42 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo zaidi ya trilioni 2.27 ni fedha za ndani na  trilioni 1.145 ni fedha za nje.

Aidha, Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, taasisi zilizo chini yake, mikoa 26 ikijumuisha halmashauri 184 imepanga kukusanya maduhuli na mapato ya ndani jumla ya zaidi ya trilioni 1.60 ikilinganishwa na trilioni 1.14 iliyoidhinishwa mwaka 2023/24, ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 456.89 sawa na asilimia 39.93.

Amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 188.96 ni makisio ya kodi ya majengo ya Ofisi ya Rais- TAMISEMI ambayo yatakusanywa na mamlaka za serikali za mitaa zilizopewa uwakala wa kukusanya kodi hiyo na kuwasilisha makusanyo hayo Mfuko Mkuu wa Serikali  huku Sh. bilioni 55.42 ni mapato ya ndani ya taasisi wakati Sh. milioni 315.93 ni maduhuli ya mikoa na Sh. trilioni 1.35 ni za mapato ya ndani ya halmashauri.

Mchengerwa amesema pia Sh. bilioni 17.79 zimetengwa kwa ajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 na kati ya fedha hizo bilioni 8 ni fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya uratibu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Makao Makuu) na Sh. bilioni 9.79 ni mchango wa halmashauri kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kugharamia uchaguzi huo. 

“Uchaguzi huu utahusu uchaguzi wa viongozi katika ngazi ya msingi ambao ni wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji, wajumbe wa halmashauri ya vijiji na wajumbe wa kamati za mitaa.”

Amesema katika mwaka 2024/25, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 357.85 za ruzuku ya fedha za maendeleo za serikali kuu na washirika wa maendeleo katika sekta ya afya.

Waziri Mchengerwa amesema pia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepanga kutumia trilioni 1.02 kupitia ruzuku ya serikali kuu na washirika wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli katika sekta ya elimu huku ikitumia Sh. bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya viongozi wa mikoa na wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya mikoa ikiwemo majengo ya utawala, ikulu ndogo, makazi ya viongozi na watumishi wa mikoa, wilaya na tarafa katika mikoa 26.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU  KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU 

    June 13, 2025
  • WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.