Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Simamieni magari yaliyotolewa kufuatilia kazi za elimu – Mhe. Mchengerwa

Imewekwa tar.: February 4th, 2024

Na. Fred Kibano, OR TAMISEMI Dodoma

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amewaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia matumizi ya magari mapya 13 yaliyotolewa na Serikali kuwa yanaleta tija ya kuwahudumia watumishi na wananchi.

Mheshiwa Mchengerwa aliyasema hayo hapo jana tarehe 03 Februari, 2024 wakati akifungua kikao kazi cha kushughulikia changamoto za upandishaji wa vyeo na kubadilisha kada kwa walimu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Mheshimiwa Mchengerwa pia amewataka viongozi hao kote nchini kuhakikisha katika taarifa zao za utendaji kazi wa kila mwezi anapata taarifa ya utendaji kazi wa Maafisa Elimu na Idara ya Afya ili kuona kama magari yaliyotolewa kwa shughuli za ufuatiliaji na utatuzi wa kero za wananchi zinafanyiwa kazi kwa wakati pamoja na Maafisa Elimu kwenda vijijini kutatua kero za walimu.

“Maafisa Elimu fanyeni mikutano na walimu, nendeni mshuke vijijini mkatatue kero na changamotoa za walimu mara moja na zile zilizo nje ya uwezo wenu kazileteni kwetu” Alisema Mheshimiwa Mchengerwa.Waziri Mchengerwa alifanya zoezi la kugawa magari 13 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.8 yatakayosaidia ufuatiliaji wa masuala ya elimu msingi katika Halmashauri 13 kupitia Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (GPE LANES II) na kuwaelekeza viongozi wa Mikoa na Wilaya kufuatilia matumizi sahihi ya magari hayo.

Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa alisema Serikali ilisaini Mradi mpya na Wadau wa GPE ambao una afua za kutatua changamoto za walimu nchini unaojulikana kama ‘Teacher Support Programme’ (TSP) wenye thamani ya shilingi Bilioni 264 ambao umeanza katika mwaka wa 2023/2024 ikiwa ni matunda ya Mheshiwa Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaimarisha mahusiano ya kimataifa na nchi na Wadau mbalimbali wa maendeleo.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa Mheshimiwa Dennis Lazaro Londo alisema magari yaliyotolewa na Programu ya Kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (GPE LANES II) yatasaidia kuhamasisha utendaji kazi na utekelezaji wa kitaaluma hasa maeneo ya pembezoni kwani yatasaidia kuongeza kiwango cha ufaulo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshiwa Rosemary S. Senyamule akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya mgeni rasmi ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Serikali na amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kuwapatia changamoto ya kwenda kufuatilia miradi ya maendeleo na kero za walimu kwani maelekezo hayo yamezaa matunda kwa kuwa ufanisi unaonekana kwa kukamilika miradi ya maendeleo na kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi na sasa kama mkoa wameandaa Mpango Mkakati wa Elimu wa mkoa na ataukabidhi kweke rasmi.

Naye Peter Fusi Afisa Elimu (Msingi) Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari kupitia Programu ya GPE kwani yeye ndiye sauti yao kwa Wadau wa Maendeleo na sasa wataweza kufika maeneo korofi kama yale yanayozunguka Mto Ruaha na Bwawa la Mtera.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.