• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali yaagiza ujenzi wa shule 232 za sekondari kukamilika kwa wakati

Imewekwa tar.: November 9th, 2022

Na Fred Kibano

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Angellah Kairuki ametoa maagizo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya shule za Sekondari 232 unakamilika kwa wakati.

Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nne wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara, leo tarehe 09 Novemba, 2022 katika Ukumbi wa Masista wa Shirika la Ivrea Jijini Dodoma.

Waziri Kairuki amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe Wakurugenzi wa Halmashauri wanakamilisha ujenzi wa madarasa 8,000 yenye thamani ya shilingi milioni 470 kwa kila shule ya sekondari unakamilika kabla au ifikapo tarehe 15 Disemba, 2022 ili kuwezesha wanafunzi wote watakaofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022 wanajiunga na Kidato cha kwanza Januari, 2023.

Aidha, amesema kupitia mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia mradi wa BOOST itajenga zaidi ya madarasa 9,000 nchini kote na kutoa rai kwa wajumbe wa kikao pindi mradi huo utakapofika katika maeneo yao kuhakikisha wanasimamia ujenzi na ukarabati wa shule za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu ili Serikali iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.  

“Serikali imezindua mradi mpya utakaotekelezwa kwa miaka 5 wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi, Tanzania Bara (BOOST) kwa gharama ya shilingi 1.15 Trilioni, mojawapo ya afua zitakazotekelezwa kupitia mradi huu ni ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi zenye uhitaji mkubwa zaidi” amesema Kairuki.

Akiongea katika mkutano huo akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amewapongeza Viongozi hao kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kusimamia miradi mikubwa ya Kukuza Stadi za Kujua Kusoma na Kuandika (GPE LANES) na Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika maeneo yao lakini pia kusimamia madarasa 15,000 ya shule za msingi na madarasa ya shule shikizi mwaka 2021.

Awali akitoa hotuba kabla ya mgeni rasmi, Rehema Ramole Mwenyekiti wa TAPSHA Tanzania Bara ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa posho kila mwezi kwa Walimu Wakuu lakini pia wanakabiliwa na changamoto ya kutengewa fedha kidogo za ujenzi ambazo hazitoshelezi kumaliza miradi wanayopewa, mlundikano wa wanafuzi na pia kuingiliwa na Maafisa wa Halmashauri kwenye michakato ya miradi ya ujenzi.

Naye Mdachi Mwanyani Mwenyeviti wa TAPSHA Halmashauri ya Chalinze amesema mkutano huo utamsaidia kutatua changamoto ya matumizi ya fedha, matumizi ya ‘force account’ na ujenzi wa madarasa chini ya Mradi mpya wa Boost.

Mkutano huo una kauli mbiu yake inayosema: “Ongezeko na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu nchini unaimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji pamoja na kuchochea ongezeko la Uandikishaji wa wanafunzi”



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.