Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mwanza, Arusha wang’ara riadha mita 800 UMITASHUMTA

Imewekwa tar.: June 28th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Wanariadha Damian Christian wa Arusha na Lucia Nestory wa Mwanza wamefanikiwa kushinda fainali za mbio za mita 800 kwa wavulana na wasichana katika mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Damian alitumia dakika 2:05:11 kujishindia medali ya dhahabu katika fainali hizo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na mkimbiaji Tilulu masanja kutoka mkoa wa Morogoro ambaye alitumia dakika 2:05:32, huku mshindi wa tatu katika mbio hizo akiwa ni Masanja Ngado kutoka mkoa wa Tabora ambaye alitumia dakika 2:05:41 na hivyo kufanikiwa kushinda medali ya shaba.

Kwa upande wa wasichana Lucia wa Mwanza aliyejishindia medali ya dhahabu alitumia dakika 2:21:00, ambapo nafasi ya pili pia ilichukuliwa Salima Mussa pia kutoka Mwanza ambaye alitumia dakika 2:21:16, na nafasi ya tatu ilishikwa na Nyanzobe Mrahi kutoka mkoa wa Mara ambaye alitumia dakika 2: 22:80

Katika fainali za mita 200 kwa wavulana ambazo pia zilifanyika leo asubuhi, nafasi ya kwanza ilishikwa na mkimbiaji Steven Stephano wa Tabora ambaye alitumia muda wa sekunde 24:58 na hivyo kujitwalia medali ya dhahabu, nafasi ya pili ilichukuliwa na mwanariadha Hamis Hussein wa Geita aliyetumia muda wa sekunde 24:97, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Daniel Emanuel wa Mwanza aliyetumia dakika 25:09.

Kwa wasichana, nafasi ya kwanza katika mbio za mita 200 ilichukuliwa na Shija Donard wa Mwanza ambaye alikimbia kwa muda wa sekunde 27:94, nafasi ya pili ilishikwa na Bertha Doto wa Geita aliyetumia sekunde 28:40, na nafasi ya tatu ilienda kwa mwanariadha Emiliana Ndele wa Mbeya ambaye alitumia  sekunde 28:45.

Katika fainali za mbio za kupokezana kijiti mita 100 x 4 kwa wavulana nafasi ya kwanza imechukuliwa na mkoa wa Mwanza ambapo washiriki wake walitumia jumla ya sekunde 47:94, nafasi ya pili imechukuliwa na mkoa wa Tabora ambapo wanariadha wake walitumia sekunde 50:19, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na washiriki kutokamkoa wa Mara ambapo walitumia sekunde 51:00.

Kwa wasichana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na washiriki wa mkoa wa Mwanza, wakifuatia na mkoa wa Mara na nafasi ya tatu imeshikwa na mkoa wa Geita. Wanariadha wa Mwanza walitumia jumla ya sekunde 54:78, Mara walitumia sekunde 55:15 na Geita walitumia sekunde 57:25.

Katika mashindano ya kuruka chini kwa wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanariadha Laurent Robert wa mkoa wa Geita ambaye alijishindia medali ya dhahabu baada ya kuruka urefu wa mita 5 na sentimita 57, nafasi ya pili ikienda mkoa wa Mwanza ambapo mwanariadha wake Kamdi Momona aliruka urefu wa mita 5 na sentimita 50, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Leonard Vises kutoka mkoa wa Shinyanga ambaye  aliruka urefu wa mita 5 na sentimita 47.

Kwa upande wa wasichana katika mchezo wa kuruka chini nafasi ya kwanza ilinyakuliwa na Mosha Julius wa Mwanza ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 57, nafasi ya pili ilichukuliwa Eliza Keraju kutoka mkoa wa Mara ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 42, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Shija Donard ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 42.

Katika mchezo wa kurusha kisahani kwa upande wa wavulana, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Kelvin John kutoka mkoa wa Mara ambaye alitwaa medali ya dhahabu aliyefanikiwa kurusha umbali wa mita 25 na sentimita 98, nafasi ya pili ikichukuliwa na Sadiki Mgale wa Songwe ambaye alirusha umbali wa mita 23na sentimita 73 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Njendage Njanje wa Manyara aliyerusha umbali wa mita 23 na sentimita 23.

Kwa wasichana, mshindi wa kwanza ni Debora Dambela wa Manyara ambaye alirusha kisahani umbali wa mita 20 na sentimita 46, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mariam kumge wa Simiyu ambaye alirusha umbali wa mita 19 na sentimita 62, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Shija Donard wa Mwanza ambaye alirusha umbali wa mita 19 na sentimita 59.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.