Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mhe. Chatanda ashuhudia utiaji saini wa Bilioni 13.3 kuboresha miundombinu Rufiji, Mhe. Mchengerwa azindua Ligi ya ”Mchengerwa Mtu Kazi”.

Imewekwa tar.: May 8th, 2025

Na John Mapepele

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya bilioni 13.3 zilizotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja wilayani Rufiji, huku Mhe. Mchengerwa akizindua rasmi Ligi ya ”Mchengerwa Mtu Kazi” inayoanza leo Mei 8, 2025 na kutoa vifaa (jezi na mipira) kwa timu zote 169 kutoka kwenye kata 13 zinazoshiriki mashindano hayo vyenye gharama ya milioni 67 pamoja na fedha taslimu milioni 25 ikiwa ni zawadi za washindi.

Tukio hili la utiaji saini limefanyika Mei 7, 2025 mara baada ya kukamilika kwa ziara ya siku mbili ya Mhe. Chatanda kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo, katika eneo la uwanja wa stendi wa Ikwiriri  na kushuhudiwa  na maelfu ya wananchi wa wilaya  hiyo huku wasanii kadhaa wakitumbuiza kwa burudani za muziki.

Akitoa taarifa ya miradi hiyo, Meneja wa Wakala za Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Pwani, Leopold Runji amefafanua kuwa gharama hizo zinahusisha ukarabati wa barabara ya Nyamwage yenye Kilomita 28, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Chumbi- Kiegele yenye kilomita 1.4, ukarabati wa barabara ya Mohoro- Mtanga kilomita 12.3 na Mohoro Ndundutawa yenye kilomita 7.5.

Pia ukarabati wa barabara ya Nyamwage- Mpakani- Nambunju na ujenzi wa  barabara za lami katikati ya mji wa Ikwiriri ambapo amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia  kuiunganisha  wilaya  hiyo na maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania.

Mhe. Chatanda amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za miradi na kufafanua kwamba  kwa kufanya hivyo siyo tu ametekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mafanikio  makubwa  bali ameleta  mapinduzi katika  sekta  ya miundombinu kote nchini.

Amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi  yote   kwa kiwango  cha juu huku akitoa wito  kwa maeneo  mengine nchini kuiga utekelezaji huo.

”Ndugu zangu hapa ni vema tuwe wakweli, unaweza ukaletewa  fedha  za maendeleo  lakini ukashindwa kutekeleza lakini,hivyo nampongeza  mbunge wenu kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hii ambayo inakwenda kuleta tija kubwa kwa wananchi  katika Wilaya ya Rufiji” amefafanua Mhe. Chatanda

Mbali na  kukagua  miradi  ya Serikali pia ameshuhudia ujenzi wa  nyumba ya mtumishi  wa chama, pia ameshuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa  wa wilaya unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.5 unaofadhiliwa na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa kwa kupitia marafiki na wadau mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu miradi ya elimu katika wilaya hiyo, Mhe. Chatanda amesema amefurahishwa na kazi nzuri ya ongezeko kubwa la Shule za Msingi na Sekondari na kutoa wito kwa wananchi kuwapeleka watoto wao  katika shule  hizo ili kuunga mkono  maono ya Mhe. Rais ya kuwakomboa wananchi kielimu pia kwa manufaa makubwa ya taifa na vizazi vyao.

Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa  amesisitiza kuwa Serikali imefanya  kazi kubwa ya ujenzi wa shule ambapo amesema  wakati anaingia kwenye ubunge kulikuwa na  na Shule za Msingi 40 tu ambapo sasa kuna shule 63 na upande wa Vituo vya Afya, awali  kulikuwa na vituo 3 na sasa  vimefika 9, huku asimshukuru Mhe. Rais Samia kwa maono makubwa  ya kuwaletea  maendeleo watanzania.

Aidha, Mhe. Chatanda alipotembelea  na  kukagua  ukarabati wa hospitali ya Wilaya  ya Rufiji na ujenzi wa kichomea taka  katika eneo la Utete  uliogharimu  takribani  milioni 900  na kuwataka  wananchi kutumia  huduma hizo ikiwa ni pamoja na wanaume kuwa msitari wa mbele kuwapeleka wake zao  kwenye  huduma za kliniki ili kujua afya za wenza wao na watoto.

Akizungungumzia kuhusu ukatili wa kijinsia, amewataka wazazi  kuwalea watoto wao katika misingi maadili  ili waweze kuja  kuwa wazazi  bora badala ya kuwaacha  kujifunza kwenye  mitandao.

Wakati huo huo ametoa wito  kwa wananchi  kujitokeza kwa wingi kujiandikisha  na kupiga kura huku akisisitiza  kuchagua CCM kwa kuwa ndicho  chama kilichowaletea  maendeleo.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • FANYENI MSAWAZO SAHIHI WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA KATIKA HALMASHAURI ZENU – MHE. DKT. DUGANGE 

    June 10, 2025
  • MHANDISI SEFF AWATAKA MAKANDARASI MIRADI YA DHARURA (SERC)KUZINGATIA MASUALA YA USALAMA KAZINI NA UTUNZAJI MAZINGIRA.

    June 10, 2025
  • Vumbi Latimuka UMITASHUMTA Iringa: Dodoma, Songwe Zatingisha katika Mpira wa Mikono

    June 10, 2025
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025

    June 09, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.