Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI KUHARAKISHA TIJA KWA WANANCHI- MHE. KATIMBA.

Imewekwa tar.: December 4th, 2024

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba (Mb) amemtaka Mkandarasi na Mtaalamu Mshauri anayetekeleza Mkataba wa Ujenzi wa miundombinu inayoratibiwa na mradi wa TACTIC wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kukamilisha haraka ujenzi huo kulingana na matakwa ya mkataba ili wananchi wanufaike kikamilifu na uwekezaji huo unaosimamiwa na Serikali kupitia TAMISEMI.

Naibu Waziri Katimba amesema hayo  leo Disemba 04, 2024 Mjini Kahama, Shinyanga, wakati wa utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi eneo la Mbulu, Ujenzi wa Soko la Sango pamoja na ujenzi wa kituo kidogo cha Mabasi na Soko la Wajasiriamali wadogo eneo la Zongomera Wilayani Kahama, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kunaenda kukuza na kuimarisha uchumi wa mwananchi na kukuza pato la Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Katimba ametoa kauli hiyo mara baada ya kupata malalamiko kadhaa kutoka kwa Viongozi mbalimbali mkoani Shinyanga, wakilalamikia mwendo usioridhisha wa Mkandarasi M/S Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation Ltd anayetekeleza ujenzi wa barabara za Mjini, Barabara ya kuingia kituo cha Wajasiriamali cha Zongomela pamoja na mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua kwenye Halamshauri ya Mji wa Kahama.

Kufuatia maelekezo hayo, Mhe. Katimba ametembelea na kukagua miradi hiyo inayolalamikiwa na kupata maoni ya wadau mbalimbali, akiahidi Kumshauri Waziri wa nchi- TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa(Mb) kuhusu hatua za kuchukua kwa Mkandarasi huyo anayesuasa katika utekelezaji wa mradi huo kwa kwenda kinyume na Mkataba na hivyo kusababisha kuchelewa kwa tija ya uwekezaji huo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Katimba amemuagiza Mtaalamu mshauri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama kuhakikisha kuwa mikataba inasimamiwa vizuri ili kuwezesha kukamilika ndani ya muda uliopangwa, kwa ubora tarajiwa huku thamani ya fedha iliyotumika ikitakiwa kuonekana kwa ukamilifu wake.

Aidha Mhe. Katimba alisema uboreshaji wa miundombinu ya barabara unaofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia TARURA, umepelekea ongezeko kubwa la bajeti ya  TARURA  kutoka Bilioni 275 hadi Bilioni 710 kwa mwaka ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 inayoelekeza kuhusu maboresho ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea shughuli za kiuchumi.

Mhe. Katimba pia  amesema uboreshaji huo umewezeshwa na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya dunia yenye kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo ya TACTIC suala linalosaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, kuibua fursa mpya za ajira pamoja na kustawisha pato la wananchi na la Manispaa, miji na Majiji ya Tanzania.

Kufuatia jitihada hizo,  Mhe. Katimba amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine inapotekelezwa  miradi ya TACTIC kulinda miundombinu hiyo ili kuhakikisha kuwa inatumika na jamii kwa muda mrefu.

" Wananchi tuna wajibu wa kuilinda miradi hii inayojengwa kwa gharama kubwa ili  kuleta tija kwa wananchi kulingana na matarajio na malengo ya mikataba ya utekelezaji wa miradi," lisema Mhe. Katimba

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.