Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

JAFO: Wakurugenzi simamieni matumizi sahihi ya fedha za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Imewekwa tar.: September 27th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi fedha zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua semina ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi  wa Halmashauri na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa  iliyofanyika katika Ukumbi  wa Auditoriumn, Chuo Kikuu cha Dodoma, Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua Wakurugenzi ambao wataenda kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa kukuika miongozo iliyotolewa na Serikali katika matumizi sahihi ya fedha hizo.

Mhe. Jafo ameonya matumizi yasiyofaa kwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kusisitiza kuwa fedha hizo ni za moto, hivyo matumizi yake yanahitaji kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa na Serikali.

Ameendelea kusema kuwa ni marufuku kwa Mkurugenzi kutumia fedha za uchaguzi kinyume na agenda ya uchaguzi na kusisitiza haja ya fedha hizo kutumika kwa wakati.

“Naomba niwape tahadhari, katika matumizi ya fedha ya uchaguzi, fedha hizi za uchaguzi zinazokuja ni kwa ajili ya uchaguzi, naomba mtu asidanganyike wala kurubunika kwa lolote katika mchakato huu wa uchaguzi, katika fedha za moto hizi fedha za moto” Amesisitiza Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inasimamia kwa karibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo ni matumaini kuwa matumizi ya fedha za uchaguzi zitaenda kama ilivyokusudiwa kwa kufuata miongozo ya matumzi ya fedha hizo.

Amesema kuwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini  ndio wenye dhamana ya kusimamia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kinyume na hapo anapaswa kujibu hoja zitakazojitokeza za kushindwa kusimamia fedha hizo vizuri.

Kuhusu wasimamizi wa uchaguzi, Mhe. Jafo amewasihi kutekeleza makujukumu yao kwa weledi na kuhakikisha ratiba ya uchanguzi inafuatwa huku akiwataka kutambua kuwa wasimamizi wamebeba dhamana kubwa katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia Demokrasia.

“ Natamani sana mlioteuliwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi mwende vizuri mpaka mmalize vizuri kwa mujibu wa kanuni zetu. Mheshimiwa Rais anatamani nchi yake ikatekeleze demokrasia vizuri na ndio maana mnaona ameweza kuwezesha kila eneo kwa lengo kuwa uchaguzi uende ukafanyike vizuri”. Amesema Mhe. Jafo

Amesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini ni muhimu kwa kuwa maisha ya watu yanaanzia katika vitongoji, mitaa na vijiji vyenu, mustakabali wa kuchakata maendeleo lazima uanze katika ngazi husika ambayo uchaguzi huu unaenda kuwapata viongozi na  hawawezi  kupatikana kama wasimamizi wa uchaguzi mtashindwa kufanya kazi yenu vizuri.

Wakati Huohuo, Mhe Jafo amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa ambao ndio waratibu wakuu wa uchaguzi kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu kila tukio na kuwataka wasikubali kuharibiwa kazi.

 “Makatibu Tawala wa Mikoa wao ni waratibu wakuu wa Uchaguzi katika Halmashauri zao kipindi hiki mna kazi kubwa sana ya kuhakikkisha huko chini mambo yanaenda vizuri na wala msikubali hata kidogo mtu awaahiribie kazi”. Amesisitiza Mhe. Jafo

Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga kukumbushana majukumu ya uchaguzi huo na kuna matukio mbalimbali yaliyopo katika tangazo la uchaguzi yanayopaswa kutekelezwa.

Mhandisi Nyamhanga amesema OR-TAMISEMI imeshakamilisha maandalizi yote muhimu ya uchaguzi huo na nyaraka mbalimbali zimeandaliwa na kusambazwa ikiwemo kanuni na muongozo wa uchaguzi huo.

Amesema tayari  imeratibu upatikanaji wa fedha na tayari zimeshatumwa kwenye Sekretarieti za Mikoa yote na anaamini zimeshatumwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya maandalizi.

Aidha, Nyamhanga alisema katika uchaguzi wa mwaka huu inakadiriwa kuwa na vituo vya kupigia kura 110,000.

Na. Angela Msimbira OR -TAMISEMI

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MWANZA YAIADHIBU PWANI SOKA MAALUMU WASICHANA

    June 12, 2025
  • SANAA ZA MAONESHO ZAANZA RASMI UMITASHUMTA 2025 MKOANI IRINGA

    June 11, 2025
  • KILIMANJARO, RUVUMA NA NJOMBE MABINGWA RIADHA MAALUMU UMITASHUMTA 2025

    June 11, 2025
  • Mtwara Wasichana Yaendeleza Ubabe UMITASHUMTA 2025

    June 11, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.