Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo awaagiza Wakurugenzi kutenga bajeti kwa ajili ya maafisa elimu maalum na elimu ya watu wazima nchini

Imewekwa tar.: August 21st, 2019


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha wanawezesha maafisa elimu nchini kwa kutenga bajeti  kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Elimu Mikoa, Maafisa elimu maalum na maafisa elimu ya watu wazima kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha mipango, Jijini Dodoma.

Amesema kuwa baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri hawatoi  kipaombele  katika masuala yanayohusu elimu maalum na elimu ya watu wazima katika Halmashauri zao jambo ambalo linafanya maafisa wa idara hizo  kuwa wanyonge na kukata tamaa ya kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

“Maafisa elimu wanaosimamia elimu maalum na elimu ya watu wazima  wako choka mbaya katika Halmashauri nyingi nchini, hata ukihesabu na kutaka viongozi wa Halmashauri wengi hawasimami kwa sababu ya kutojiamini na kujiona wametengwa na jamii hii inaleta sura mbaya na kusababisha watu walioko kwenye kundi hili kusahaulika  na kutotimiziwa mahitaji yao kwa wakati” Amesema Jafo.

Mhe. Jafo anafafanua kuwa maafisa elimu maalum  na elimu ya watu wazima hushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kutotengewa fedha na kuonekana si vipaombele vya Halmashauri, jambo ambalo linasababisha watoto wengi wenye mahitaji maalum na watu wazima kushindwa kupata elimu bora sawa na watu wengine.

“ Afisa elimu maalum akiwa na kazi maalum lazima aombe msaada wa gari kutoka Idara nyingine,hivyo nawaagiza wakurugenzi kuhakikisha katika bajeti zenu za ndani kutenga fedha kwa ajili ya maafisa elimu maalum na elimu ya watu wazima ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo” Amesisitiza Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amewataka kuhakikisha wanaainisha vipaombele vya elimu maalum na watu wazima na kuviingiza katika bajeti ya Halmashauri husika ili kuziwezesha Idara hizo kupanga mipango yao na kuitekeleza kwa wakati.

Wakati huohuo, amemuagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha kila Halmashauri  inaainisha kwenye bajeti zao  vipaombele vya  Elimu Maalum na Elimu ya watu wazima  katika mchakato mzima wa bajeti  na kuwekewa fungu  katika Halmashauri zote nchini.

Amemtaka kuhakikisha anafanya uhakiki kwa kila mkoa pindi inapoleta bajeti yake kama wameweka vipaombele vya elimu maalum na elimu ya watu wazima, kama ilivyofanywa kwa asilimia kumi ya kuwawezesha vijana, wanawake na walemavu ili kuyafikia makundi hayo.

Mhe. Jafo amesema bila kufikia mahali na kuona ni kipaombele cha Halmashauri kuhakikisha kundi la watu maalum na elimu ya watu wazima linahudumiwa katika jamii, kundi hili litakuwa likitegemea wafadhili pekee jambo ambalo si malengo ya Serikali.

Vilevile amewaagiza maafisa elimu Maalum na watu wazima kuhakikisha wanatembelea maeneo yao ya kazi ili kutatua matatizo  ya kundi hili katika maeneo wanayofanyia kazi.

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa malengo ya mkutano huu ni  kuwapa uelewa Maafisa elimu kuhusu mpango mkakati wa elimu jumuishi kuwa ni ajenda muhimu katika maeneo yao ya kazi, kuwajengea uwezo wa namna ya kukuza na kusimamia maadili ya uongozi wa utumishi wa umma na dhana nzima ya ugatuaji wa madaraka na  kuendesha na kusimamia programme mbalimbali za maendeleo ya elimu nchini.

 Aidha, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Tixon Nzunda amewaomba wadau wa elimu nchini kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake katika kutatua changamoto mbalimbali za elimu nchini kwa kufuata vipaombele vinavyotolewa na kinyume chake watapingana na juhudi za Serikali.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.