Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo atolea ufafanuzi malalamiko yaliyowasilishwa kwenye zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu

Imewekwa tar.: October 30th, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo ametolea maelekezo malalamiko yaliyowasilishwa na wadau wa uchaguzi kuwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi uzingatie Kanuni za uchaguzi na miongozo iliyotolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jioni la leo Ofisini kwake Mtumba Jafo ameelekeza Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi, Vyama vya Siasa na wadau wengine woote kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anazingatia masharti na miongozo iliyotolewa kuhusiana na uchukuaji na urejeshaji wa fomu.

Amebainisha baadhi ya malalamiko yaliyowasilishwa toka kwa vyama vya siasa kuwa ni kutokuwepo vituoni kwa baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi, baadhi ya wasimamizi kutofungua kwa wakati vituo vya kuchukulia fomu, mihuri na masuala mengine ya Kikanuni.

“Malalamiko yaliyopokelewa yanaendelea kufanyiwa kazi, hata hivyo wadau na vyama vya siasa wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwenye kamati za rufaa zilizopo katika maeneo ya uchaguzi,” alibainisha.


Akieleza maendeleo ya uchaguzi huo jana jijini hapa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, alisema dosari zilizojitokeza ni chache kwenye baadhi ya mikoa.

Alisema katika Kata 3,959 ni kata 72 pekee ndizo amepokea malalamiko na kutaja maeneo machache kama vile Songwe, Lindi, Sengerema (Mwanza) na Moshi (Kilimanjaro).

Hata hivyo, Jafo alisema malalamiko kuhusu fomu zinazotolewa kwa wagombea kutogongwa muhuri, vyama vya siasa vinapaswa kufahamu kuwa, zitagongwa muhuri   pindi watakaporudisha au wakati wa uteuzi.

Kadhalika, alitoa msisitizo kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi kuzingatia kanuni za uchaguzi kama zilivyowekwa.

Juzi, Waziri Jafo alitangaza wagombea kwenye uchaguzi huo kuanza kuchukua fomu kwenye ofisi za wasimamizi wa uchaguzi hadi Novemba nne mwaka huu.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti wa Mtaa, Kitongoji, Kijiji, Wajumbe wa Kamati ya  Mtaa, Waju,mbe wa Serikali ya Kijiji.

Uchaguzi huo ambao ni wa sita tangu kuanza mfumo wa vyama vya siasa nchini, unatarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu ambapo wapigakura zaidi ya milioni 19 wanatarajiwa kushiriki


Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.